Leo magazeti na watangazaji wa khabari wanatangaza kuchukua maoni mbalimbali na kuwapanulia watu na kuwa wakirudishwa katika dalili kuna neno na kwamba ni kuwabana. Wanasema namna hii. Hii ni kufuru. Kwa sababu mwenye kuyasema anaonelea kuwa kutendea kazi dalili kuna neno. Mwenye kusema hivi anakufuru. Kutendea kazi dalili ni faraja na sio neno. Ni wepesi kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
Haya ndio maneno juu ya masuala haya yanayohusiana na tofauti za wanazuoni na ni maoni yepi yanayotakiwa kutendewa kazi juu ya masuala yenye makinzano.
Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakika maneno ya Mtume wa Allaah ni takasifu… ”
Maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio yenye kuzingatiwa. Yeye ndiye ambaye tumeamrishwa kumfuata. Hatukuamrishwa kufuata maoni ya yeyote. Wanazuoni wanatadharisha haya kweli kweli.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 195-196
- Imechapishwa: 13/01/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)