Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Na wala masikini huyu hajui kuwa wengi wa viongozi waliokufuru wanaijua haki na wanaiacha kwa sababu ya udhuru fulani. Kama alivyosema (Ta´ala):
اشْتَرَوْا بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا
“Wamebadili Aayah za Allaah kwa thamani ndogo.” (09:09)
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ
“Wale Tuliowapa Kitabu wanatambua kama wanavyotambua watoto wao.” (02:146)
MAELEZO
Masikini huyu haelewi kuwa viongozi wengi wa kufuru waliitambua haki. Pamoja na hivyo wakafanya jeuri na kwenda kinyume na haki. Amesema (Ta´ala):

“Wale Tuliowapa Kitabu wanatambua kama wanavyotambua watoto wao.”

“Wamebadili Aayah za Allaah kwa thamani ndogo.”
Walikuwa wakija na nyudhuru zisizokuwa na maana. Walikuwa wakisema kuwa wanakhofia wasije kukosa nafasi zao za uongozi na mfano wa hayo.
Viongozi wengi wa kufuru wanajua haki, lakini hawaifuati na wanaichukia. Kuitambua haki pasi na kuitendea kazi ni kubaya zaidi kuliko kutoitambua. Mjinga anapewa udhuru. Mtu kama huyu afunzwe ili azindukane na kujifunza. Hili ni tofauti na mtu mkaidi na mwenye jeuri. Ndio maana mayahudi wakawa ni wenye kughadhibikiwa. Waliitambua haki na wakaacha kuifuata. Upande mwingine manaswara wakawa wapotevu kwa sababu hawakuijua haki. Lakini baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutumwa, manaswara pia wakaitambua haki na hivyo na wao pia wakawa ni wenye kughadhibikiwa kama mayahudi.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 101-102
- Imechapishwa: 28/11/2023

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 101-102
Imechapishwa: 28/11/2023
https://firqatunnajia.com/93-mlango-wa-16-viongozi-wengi-wa-kufuru-wanaitambua-haki/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)