Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Amesema tena:

“Nywele zake timtim na miguu yake imeingia vumbi. Ananyoosha mikono yake kuelekea mbinguni akisema: “Ee Mola! Ee Mola!”[1]

MAELEZO

Hadiyth hii inahusu yule msafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi watu! Hakika Allaah ni mzuri na wala hakubali isipokuwa kilicho kizuri. Allaah amewaamrisha waumini yale aliyowaamrisha Mitume. Akasema:

يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ

“Enyi Mitume! Kuleni katika vizuri na tendeni mema – hakika Mimi kwa yale myatendayo ni Mjuzi.”[2]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ

“Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni.”[3]

Baada ya hapo akamtaja bwana mmoja ambaye amesafiri safari ndefu. Nywele zake zimekuwa timtim na miguu yake imeingia vumbi. Ananyoosha mikono yake kuelekea mbinguni akisema: “Ee Mola! Ee Mola!” Chakula chake ni cha haramu, mavazi yake ni ya haramu na amekulia juu ya haramu; ni vipi ataitikiwa?”

Anamnyooshea mikono Allaah (Jalla wa ´Alaa), kwa sababu Allaah yuko juu ya mbingu. Anamnyooshea mikono Allaah, Aliye juu, akisema:

“Ee Mola! Ee Mola!”

Anakariri du´aa yake na akifanya king´ang´anizi, jambo ambalo ni miongoni mwa sababu za kuitikiwa du´aa. Hata hivyo licha ya kuwa yuko na sababu hizi za kuitikiwa du´aa – yuko safarini, mazingira yake ni mabaya kutokana na safari, ananyoosha mikono yake kuelekea mbinguni na anaikariri du´aa yake na kung´ang´ania – du´aa yake haijibiwi. Kikwazo ni “chakula chake ni cha haramu, mavazi yake ni ya haramu na amekulia juu ya haramu”. Hakula chakula kizuri na chenye kunufaisha. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ

“… anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharamishia vichafu… ”[4]

Huyu hakula katika vilivyo vizuri. Ndio maana du´aa yake haikuitikwa. Jumla isemayo ”Ananyoosha mikono yake kuelekea mbinguni akisema: “Ee Mola! Ee Mola!” inathibitisha kuwa Allaah yuko juu ya viumbe Wake.

[1] Muslim (1015).

[2] 23:51

[3] 2:172

[4] 7:157

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 134-135
  • Imechapishwa: 28/08/2024