92. Mtume akiwa kuliani mwa ´Arshi

89 – ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtu wa kwanza atakayevishwa nguo ni Ibraahiym – nguo mbili za kikoptiki. Kisha avishwe nguo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) joho, suti ya kiyemen. Atakuwa upande wa kuliani mwa ´Arshi.”[1]

Haya ni masimulizi ya Swahabah.

[1] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Ameitaja katika asili, uk. 85, kupitia kwa Sufyaan ath-Thawriy, kutoka kwa ´Umar bin Qays, kutoka kwa al-Minhaal bin ´Amr na ´Abdullaah bin al-Haarith, kutoka kwake. Ibn-ul-Mubaarak ameipokea katika “az-Zuhd” (364). Därtill har den följts upp av Muhammad bin ´Abdillâh bin az-Zubayr. Isitoshe amefuatiliwa na Muhammad bin ´Abdillaah bin az-Zubayr, aliyesimuliwa na Sufyaan.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 109
  • Imechapishwa: 05/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy