Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah ni Mwingi wa hayaa na Mkarimu. Anamuonea hayaa mja Wake anamponyanyulia mikono kuirudisha bure.”[1]

MAELEZO

Hadiyth hii inamthibitishia Allaah kuona hayaa. Hayaa ni sifa nzuri ambayo Allaah anasifiwa nayo vile inavyolingana na utukufu Wake. Hayaa hiyo sio kama hayaa ya viumbe. Allaah anaghadhibika, lakini sio kama kughadhibika kwa viumbe. Allaah anaridhia, lakini sio kama kuridhia kwa viumbe. Anachukia, lakini sio kama kuchukia kwa viumbe. Kwa hivyo Allaah anasifiwa kuona hayaa pia, lakini ni hayaa maalum na inayolingana Naye (Subhaanahu wa Ta´ala).

Anaona hayaa (Subhaanahu wa Ta´ala) mja Wake kumnyooshea mikono akimuomba du´aa ambapo akairudisha mitupu. Bali (Subhaanahu wa Ta´ala) anamuitikia anayemuomba na akamnyooshea mikono. Vilevile Hadiyth inathibitisha kuwa yuko (Subhaanahu wa Ta´ala) juu, kwa sababu mikono kunyanyuliwa juu kunaashiria ujuu.

[1] Abu Daawuud (1488), at-Tirmidhiy (3556) aliyesema kuwa ni nzuri na geni, Ibn Maajah (3865) na al-Haakim (1/675).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 133
  • Imechapishwa: 27/08/2024