´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) alipokuwa akisimama karibu na kaburi alikuwa akilia sana mpaka ndevu zake zinaloa. Akaambiwa: “Hulii pindi unapofikiria Pepo na Moto na unalia kwa sababu ya hili.” Akasema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kaburi ndio kituo cha kwanza cha Aakhirah. Mwenye kusalimika nayo yote yaliyo baada yake yatakuwa ni mepesi kwake. Asiyesalimika nayo yote yaliyo baada yake yatakuwa magumu.”[1]
at-Tirmidhiy amepokea kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Sijapatapo kuona muonekano isipokuwa kaburi linatisha kuliko wenyewe.”[2]
Mujaahid amesema:
“Kitu cha kwanza kinachomzungumzisha mwanaadamu ni kaburi lake. Humwambia: “Mimi ndio nyumba ya minyoo. Mimi ndio nyumba ya upweke. Mimi ndio nyumba ya faragha. Mimi ndio nyumba ya giza. Mimi ndio nyumba ya ugeni. Ee mwanaadamu! Haya ndio niliyokuandalia. Wewe umeniandalia nini?”
Abud-Daraa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Nisikuelezeni siku ya ufakiri wangu? Ni ile siku nitayoingizwa ndani ya kaburi langu.”
Ja´far as-Swaaqid (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akiyatembelea makaburi usiku na kuyaambia:
“Enyi mlio ndani ya makaburi! Kwa nini hamniitikii ninapowaita? Ninaapa kwa Allaah kuwa hawawezi kuitikia. Ni kama mimi ni mmoja katika wao.”
Halafu anaelekea Qiblah mpaka inapoingia alfajiri.
´Umar bin ´Abdil-´Aziyz alimwambia mmoja katika marafiki zake:
“Jana jioni nililifikiria kaburi na mauti. Lau ungeliyaona mauti baada ya siku tatu ungelihisi wasiwasi baada ya kuanasika nayo kwa muda mrefu. Umeona nyumba iliyojaa wanyama. Umeona maji ya majeraha yanayakimbia mauti. Umeshaona minyoo wanavyomla. Harufu imebadilika na sanda imeharibika. Yote hayo baada ya kuwa nzuri, yenye harufu yenye kunukia na iliyo nzuri.”
Kisha akapiga ukelele mpaka akaanguka na kuzimia.
Baadhi ya wenye hekima wamesema:
“Kuna bahari nne ya vitu vinne; mauti ni bahari ya uhai. Nafsi ni bahari ya matamanio. Kaburi ni bahari ya majuto. Msamaha wa Allaah ndio bahari ya madhambi. Tunamuomba Allaah Mtukufu ayafanye makaburi yetu kuwa ni majumba bora kabisa.”
[1] at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na al-Haakim.
[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (1684).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 191-193
- Imechapishwa: 02/12/2016
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
55. Kuamini mtihani, hesabu na adhabu ndani ya kaburi
Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema: Katika kuamini siku ya Aakhirah kunaingi kuyaamini yote aliyoelezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya yatakayokuwa baada ya mauti. Wanaamini mitihani ya ndani ya kaburi, adhabu ya kaburi na neema zake. Kuhusu mitihani yake ni kwamba watu watapewa mitihani ndani ya makaburi…
In "Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah - Ibn Baaz"
109. Radd juu ya uongo wa Ibn Suwhaym kwamba Shaykh anataka kubomoa kuba la Mtume
Maneno yake: “Na kwamba eti nasema laiti lingeweza kubomoa kuba la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi ningefanya hivo.” Hii ni moja katika uongo juu ya Shaykh. Kwa sababu ni jambo linalotambulika kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amezikwa kwenye nyumba yake hali ya kuwa ni…
In "´Aqiydah ya Ibn ´Abdil-Wahhaab - al-Fawzaan"
20. Makatazo ya kuabudu makaburi au kumuabudu Allaah kwenye kaburi la mtu mwema
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: 1- Imesihi kupokelewa kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia kwamb Ummah Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alimtajia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kanisa aliyoiona Habashah na namna ilivyokuwa mapicha. Akasema: “Hao ndio wale ambao wanapofiwa na mtu mwema au…
In "Sharh Kitaab-it-Tawhiyd - Ibn Baaz"