89. Wakati Ibn Rawaahah aliposhtukiziwa na kijakazi wake

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

´Abdullaah bin Rawaahah (Radhiya Allaahu ´anh) alisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Nashuhudia kwamba ahadi ya Allaah ni haki

na kwamba Moto ni makazi ya makafiri

na kwamba ´Arshi iko juu ya maji

na kwamba juu ya ´Arshi yuko Mola wa walimwengu

inabebwa na Malaika watukufu

na Malaika wa Mungu ni wenye kuleta upepo

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkubalia maneno yake[1].

MAELEZO

Miongoni mwa maneno ya Maswahabah yanayothibitisha kuwepo juu kwa Allaah ni maneno ya ´Abdullaah bin Rawaahah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh). Alikuwa mshairi fasaha na mmoja katika washairi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aliutetea Uislamu na akawaraddi washirikina kwa mashairi yake. Kama mfano wa Hassaan bin Thaabit, Ka´b bin Maalik na Ka´b bin Zuhayr (Radhiya Allaahu ´anhum); hawa ni washairi waliyoyatumia mashairi yao kumtetea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakawaraddi washirikina.

Kisa chake ni kwamba alikuwa na kijakazi aliyekuwa akilala naye. Siku moja akaja mke wake na akashikwa na wivu kama wanawake wengine. Kwa ajili ya kuepuka matatizo, akakanusha kuwa amefanya kitu na kijakazi yule ambapo mke wake akamwambia ambaye yuko na janaba haifai kwake kusoma Qur-aan; soma Qur-aan kama kweli hujafanya kitu! Ndipo akamfanyia Tawriyah kwa njia ya kwamba akayasoma mashairi hapo juu ambapo mwanamke yule akafikiria kuwa ni Qur-aan. Mwanamke yule akamsadikisha. Hii ni Tawriyah. Inafaa kwa mtu kufanya Tawriyah akiwa si mwenye kudhulumu. Akamsadikisha na kusema kuwa anamwamini Allaah na kuyakadhibisha macho yake. Baada ya hapo tukio hilo akaelezwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akamkubalia kitendo chake.

Kinacholengwa katika mashairi hayo ni  “kwamba juu ya ´Arshi yuko Mola wa walimwengu” ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkubalia. Akamkubalia jumla inayosema kuwa ´Arshi iko juu ya maji na kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi.

[1] al-Istiy´aab kwenye ”al-Iswaabah” (2/296) ya Ibn Hajar.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 27/08/2024