Shirki ndogo inasamehewa kama madhambi mengine?

Swali: Je, shirki ndogo inasamehewa kama madhambi mengine?

Jibu: Ndio, inakusanywa na msamaha. Akitubia kutokana na shirki basi Allaah anamsamehe. Lakini asipotubia hawasamehewi kwa mujibu wa wanazuoni wakaguzi. Hata hivyo kutapimwa kati ya matendo yake mema na maovu na mema yake yakiwa na uzito zaidi basi hatochukuliwa hatua kama maasi mengine.

Swali: Nimemsikia Shaykh mmoja – kana kwamba ananasibisha kwa Shaykh-ul-Islaam – ya mtu wa shirki ndogo ataadhibiwa kwa hali yoyote ile?

Jibu: Hapana, ni kosa. Anaweza kusamehewa kutokana na mema yake. Tunamuomba Allaah msamaha. Ueneaji wa dalili zinafahamisha kuwa hasahewi isipokuwa kwa kutubia, hata hivo uhalifu na madhambi yake yanaweza kuanguka kutokana na uzito wa mema yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24096/هل-تشمل-المغفرة-صغير-الشرك-عند-التوبة
  • Imechapishwa: 26/08/2024