88- Muislamu hazikwi pamoja na kafiri wala kafiri pamoja na muislamu. Bali muislamu azikwe katika makaburi ya waislamu na kafiri katika makaburi ya makafiri. Hivo ndivo ilivyokuwa ikifanywa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hali hiyo ikaendelea mpaka katika zama zetu hizi. Miongoni mwa dalili ya jambo hilo ni Hadiyth ya Bashiyr bin al-Khaswaaswiyyah ambaye ameeleza:
“Wakati nilipokuwa nikitembea na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) [hali ya kuwa nimeushika mkono wake] akasema: “Ee Ibn-ul-Khaswaaswiyah! Kipi [kimekupelekea] kule kuhisi vibaya kwa Mola Wako?[1] Umekuwa sasa ni mwenye kutembea na Mtume wa Allaah! [Nahisi alisema: “Hali ya kuwa ni mwenye kumshika mkono wake.”] Nikasema: [“Ee Mtume wa Allaah! Namtoa fidia baba na mama yangu!] Hakuna chochote [kinachonipelekea] kuhisi vibaya kwa Allaah. Kheri zote amenipa Allaah. Akayaendea makaburi ya washirikina ambapo akasema: “Hakika watu hawa wameziacha nyuma yao kheri nyingi. [Katika upokezi mwingine imekuja: “Kheri nyingi] mara tatu.” Kisha akayaendea makaburi ya waislamu ambapo akasema: “Hakika watu hawa wamepata kheri nyingi. Akasema hivo mara tatu. Wakati alipokuwa akitembea mara ikatoka kutoka kwake ishara ya kutazama. Tahamaki akamuona mtu mmoja anatembea kati ya makaburi akiwa amevaa viatu ambapo akasema: “Ee bwana uliyevaa viatu viwili! Ole wako vua viatu vyako.” Mtu yule akatazama na wakati bwana yule alipojua kuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akavua vuatu vyake na akavitupa.”
Ameipokea Abu Daawuud (02/72), an-Nisaa´iy (01/288), Ibn Maajah (01/474), Ibn Shaybah (04/170), al-Haakim (01/373) na mtiririko ni wake na al-Bayhaqiy amepokea kupitia njia yake (04/80), at-Twayaalisiy (1123), Ahmad (05/83, 83, 84, 224) na ziada ni zake na at-Twabaraaniy (02/42/123), ya pili ni ya al-Bayhaqiy na haipo katika “al-Mustadrak”. at-Twahaawiy ameipokea (01/293) kutoka kwake kisa cha bwana huyo ambaye alikuwa amevaa viatu. al-Haakim amesema:
“Ni yenye cheni ya wapokezi Swahiyh.” adh-Dhahabiy akaafikiana naye na al-Haafidhw akamkubalia katika “al-Fath” (03/160). Ibn Maajah ameipokea kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Uthmaan, ambaye ni mtu wa Baswrah, swahiba wa Shu´bah kwamba amesema: “Hadiyth ni nzuri.”
Ameinukuu Ibn-ul-Qayyim katika “Tahdhiyb-us-Sunan” (04/343) kutoka kwa Imaam Ahmad ambaye amesema:
“Cheni ya wapokezi Swahiyh ni nzuri.”
an-Nawawiy amesema katika “al-Majmuu´” (05/412):
“Cheni ya wapokezi Swahiyh ni nzuri.”
Ibn Hazm (05/142, 143) ameijengea hoja kwamba haifai kumzika muislamu pamoja na mshirikina. Sehemu nyingine ameitumia kama hoja juu ya uharamu wa kutembea kwa viatu kati ya makaburi, kama itavyokuja katika maelezo ya masuala ya 126.
[1] Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia hivo kwa sababu Bashiyr (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa ameshaanza kudhihirisha kitu katika kujihisi vibaya kwa sababu ya kule kukaa kwake mbali na mji wa watu wao. at-Twabaraaniy amepokea katika “al-Kabiyr” na “al-Awsatw” kutoka kwa Bashiy mwenyewe aliyesema:
“Nilimwendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na nikamkuta al-Baqiy´ ambapo nikamsikia akisema:
السلام على أهل الديار من المؤمنين
“Amani ya Allaah iwe juu ya makazi haya katika waumini.”
Ukakatika mkanda wangu wa kitu ambapo akasema: “Tengeneza kiatu chako.” Nikamwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Kuishi kwangu mbali na nyumbani kumekuwa kurefu na nimekuwa mbali na mji wetu.” Akasema: “Ee Bashiyr! Kwa nini usimhimidi Allaah ambaye ameshika sehemu yako ya utosi akakutoa kutoka katika kabila la Rabiy´ah. Watu ambao wanaona kama si wao basi ingelibiduka ardhi na vilivyomo ndani yake.
al-Haythamiy amesema katika “al-Mujma´” (03/60):
“Wapokezi wake ni waaminifu.”
Kisha nikaona Hadiyth katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (02/45-46) na ”al-Awsaatw” (116- Mujma´-ul-Bahrayn) na “Taariykh Ibn ´Asaakir” (10/170) kupitia njia ya ´Utbah bin al-Mughiyrah ash-Shaybaaniy: Ishaaq bin Abiy Ishaaq ash-Shaybaaniy ametuhadithia… kutoka kwa Bashiyr kwayo. Isipokuwa yeye amesema: “Lau isingelikuwa wao… “ ´Utbah na shaykh wake Ishaaq Ibn Abiy Haatiym (03/01/316) na (01/01/223) amewawekea kichwa cha khabari na wala hakutaja ndani yake jambo la kujeruhi wala kuadilisha. Dhahiri ni kwamba Ibn Hibbaan amewafanya kuwa waaminifu. Rejea kitabu changu “ath-Thiqaat”. Kisha nikamfanya kichwa cha khabari katika “adh-Dhwa´iyfah” (6035).
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 172-173
- Imechapishwa: 16/02/2022

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 172-173
Imechapishwa: 16/02/2022
https://firqatunnajia.com/89-uharamu-wa-kuwazika-waislamu-na-makafiri-sehemu-moja/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)