Swali 89: Je, kiapo cha utiifu ni jambo la wajibu au lenye kupendeza? Ni ipi nafasi ya kiapo cha utiifu inapokuja katika mkusanyiko, kusikiliza na kutii?
Jibu: Yule mtu ambaye ameteuliwa kuwa kiongozi wa waislamu kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ni lazima kumsikiliza na kumtii. Wale watu wanaompa kiapo hicho ni wale watu wenye ushawishi katika wanazuoni na viongozi. Wananchi wengine ni wanakuwa chini ya kiapo hicho. Wanalazimika kumtii kiongozi kutokana na kiapo cha watu hawa. Kwa msemo mwingine si kila muislamu anatakiwa kutoa kiapo chake. Kwa sababu waislamu ni wamoja; viongozi na wanazuoni wanachukua nafasi zao kwa niaba yao. Hivo ndivo walivokuwa wakifanya Salaf. Namna hiyo ndivo Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) alivopewa kiapo na wengineo katika watawala wa waislamu.
Kiapo cha usikivu na utiifu katika Uislamu haiwi kwa njia ya vurugu inayoitwa uchaguzi. Chaguzi kama hizo hufanywa katika nchi za kikafiri, na nchi za kiarabu zilizowaigiliza, na ambacho kinatokana na kupakana mafuta na uwongo. Mara nyingi chaguzi hizi zinaishilia kwa umwagikaji wa damu. Kiapo cha utiifu katika Uislamu hupelekea katika umoja na muungano, amani na utulivu, bila kuwepo zabuni na mashindano ya fujo ambayo yanagharimu watu shida, ugumu, umwagikaji damu na mengineyo.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 218-221
- Imechapishwa: 30/07/2024
- Taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)