88. Ni upi wajibu wa walinganizi na wanafunzi juu ya watawala?

Swali 88: Ni upi wajibu wa walinganizi na wanafunzi juu ya watawala?

Jibu: Wajibu kwa wale wanaolingania kwa Allaah ni kufanya bidii waislamu wawe na umoja na kusambaratisha mipango ya makafiri na wanafiki. Malengo yao ni kuitawanyisha jamii ya Kiislamu, kupanda chuki na uadui kati ya waislamu na kuwatenganisha waislamu na viongozi wao. Ni lazima kwao kuwahimiza waislamu kuwa na umoja, kuungana na kuwatakia mema watawala, kuwasaidia katika haki na kuwaelekeza katika kheri pasi na kashfa wala ukemeaji[1]. Amesema (Ta´ala):

فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ

“Mwambieni maneno laini huenda akawaidhika au akaogopa.”[2]

[1] Miongozo na maelekezo haya yanatakiwa kuwa katika Khutbah za ijumaa na mihadhara yenye kuenea badala ya Khutbah na mihadhara ya hamasa na ya uchochezi inayosababisha chuki dhidi ya watawala. Madaraja yote shuleni yanatakiwa kulelewa juu ya kuwapenda na kuwaheshimu watawala kutowatia upungufu. Kwa sababu kuwatia upungufu kunapelekea kutosikilizwa na kutiiwa katika yaliyo mema. Kunapotokea mambo hayo basi kunaenea fujo na fitina. Walinganizi wanatakiwa wayajue hayo na wawaelekeze vijana kwa miongozo sahihi na iliyo salama iliyochukuliwa kutoka ndani ya Qur-aan, Sunnah na kwa ufahamu wa Salaf.

[2] 20:44

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 216
  • Imechapishwa: 30/07/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy