Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kwani kuwa na ujuzi juu ya haya ni asili ya a dini na msingi wa uongofu na pia ndio kitu bora na cha wajibu zaidi ambacho viumbe wanaweza kujichumia.
MAELEZO
Kuwa na ujuzi kuhusu ´Aqiydah ndio msingi wa dini. Yule anayefanya upungufu katika msingi huu basi amefanya upungufu katika dini. Kwa sababu kitu kikiwa na kasoro katika msingi wake basi matawi yake pia huwa na kasoro. Msingi wa nyumba ukiwa na kasoro inabomoka, na ikiwa msingi wa nyumba ni imara nyumba nayo inakuwa imara na kusimama. Nyumba mbaya hubomoka. Ni vipi basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asitilie umuhimu msingi wa dini, ambao ni ´Aqiydah, akawabainishia na kuwawekea nayo watu wazi mpaka eti waje waliokuja na kuwaletea watu ´Aqiydah kutoka vichwani mwao au kutoka kwa wengine na kuziona kuwa ni nzuri? Fikira kama hiyo ndio upotofu wenyewe na ni kupingana na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Endapo mtu atakuwa na bidii katika ´ibaadah na akafunga michana, akasimama usiku kuswali na akatoa kiasi kikubwa cha fedha lakini akawa hana ´Aqiydah sahihi, matendo yake yote ni bure na hayana maana yoyote pasi na kujali ni kiasi gani atajichosha nafsi yake kufanya ´ibaadah. Kwa hiyo ni lazima matendo na ´ibaadah zake zijengeke juu ya msingi na ´Aqiydah iliosalimika ili matendo yake yawe yenye kukubaliwa:
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا
“Hakika Allaah hadhulumu uzito wa atomu. Na ikiwa ni [kitendo] kizuri hukizidisha na hutoa kutoka kwake ujira mkubwa.”[1]
Allaah anayabariki matendo machache yaliyofanywa kwa kumtakasia Yeye (´Azza wa Jall) na yaliyosalimika kutokana na Bid´ah. Matendo kama hayo yanamfaa mtendaji. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Uogopeni Moto ijapo kwa kipande cha tende. Asiyepata kipande cha tende basi aseme neno zuri.”[2]
Matendo mema, ijapo yatakuwa machache, yamebarikiwa. Lakini matendo yasiyokuwa mema, ijapo yatakuwa mengi – hayana faida yoyote. Kwa hivyo kinachozingatiwa sio kujipinda na kufanya ´ibaadah kwa wingi, bali kinachozingatiwa ni usahihi na kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] 4:40
[2] al-Bukhaariy (3595) na Muslim (1016).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 54-55
- Imechapishwa: 30/07/2024

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 54-55
Imechapishwa: 30/07/2024
https://firqatunnajia.com/26-kuijua-aqiydah-ndio-msingi-wa-dini/