Baadhi ya vitabu vizuri katika Fiqh na Takhriyj ya al-Albaaniy

Swali: Naomba unipendekezee vitabu vya Fiqh ambavyo vinaweza kuninufaisha katika dini na dunia yangu?

Jibu: Vitabu vya Fiqh ni vingi. Miongoni mwa vitabu bora ni maelezo juu ya ”ar-Rawdhw al-Murbiy ´alaa Sharh Zaad-il-Mustaqniy´´” cha Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Qaasim. Kimeshachapishwa, kipo na ni moja katika vitabu bora kabisa. Kadhalika ”al-Muqniy´” cha Ibn Qudaamah kwa maelezo ya Sulaymaan bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh ambayo ni mazuri na yenye faida. Miongoni mwa vitabu bora pia ni ”´Umdat-ul-Fiqh” ambacho ni kifupi katika Fiqh. Kimeandikwa na ´Abdullaah bin Ahmad bin Qudaamah, mtunzi wa ”al-Mughniy´”. Moja katika vitabu bora pia ni ”Daliyl-ut-Twalab” na maelezo yake ”Manaar-us-Sabiyl”. Ndugu yetu na ´Allaamah na Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy amekifanyia Takhriyj. Vitabu vyote hivi ni vyenye faida.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.binbaz.org.sa/mat/10474
  • Imechapishwa: 17/01/2021