Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh:

“Wakati Allaah (´Azza wa Jall) alipohukumu viumbe aliandika katika kitabu Chake kilichoko Kwake juu ya ´Arshi: ”Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.”[1]

MAELEZO

Hadiyth inafahamisha kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko juu ya ´Arshi. ´Arshi ndio kiumbe kilicho juu kabisa; hakuna kiumbe chochote kilichoko juu ya ´Arshi. Allaah (´Azza wa Jall) yuko juu ya ´Arshi ujuu ambao unalingana na utukufu Wake. Haina maana kuwa anahitaji ´Arshi hiyo au kwamba ´Arshi inambeba – bali Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye ambaye anaizuia ´Arshi kwa uwezo Wake.

Hadiyth inathibitisha pia kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anaandika.

Inafahamisha pia kwamba wako baadhi ya viumbe walioko Kwake kwa njia ya nafasi na matukuzo. Kama alivosema Allaah (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ

“Hakika wale walioko kwa Mola wako hawatakabari kufanya ‘ibaadah Yake na wanamsabihi na Kwake pekee wanasujudu.”[2]

[1] al-Bukhaariy (3194), Muslim (2751), Ahmad (2/466) na wengineo.

[2] 7:206

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 127
  • Imechapishwa: 26/08/2024