86. Muumba yuko juu ya ´Arshi Yake

Katika mambo yanayofahamisha kuwa Muumba (Tabaarak wa Ta´ala) yuko juu ya kila kitu, juu ya ´Arshi Yake tukufu, na hakukita mahali popote, ni maneno Yake (Ta´ala):

وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

”Kursiy Yake imeenea mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye yujuu kabisa, Ametukuka.”[1]

وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ

”Naye Yuko juu, Mkubwa kabisa.”[2]

عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْكَبِيرُ الْمُتَعَالِ

”Mjuzi wa yaliyofichikana na yenye kuonekana, Mkubwa kabisa Aliye juu.”[3]

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

“Sabihi Jina la Mola wako Aliye juu!”[4]

Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha sisi kusema tunaposujudu:

سبحان ربي الأعلى

“Ametakasika  Mola wangu, Aliye juu kabisa.”

Amesema (Ta´ala) kuhusu mashahidi:

بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ

”Bali wahai kwa Mola wao wanaruzukiwa.”[5]

Amesema (Ta´ala) kuhusu mke wa Fir´awn:

رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ

”Mola wangu! Nijengee nyuma Kwako kwenye Pepo.”[6]

[1] 02:255

[2] 34:23

[3] 13:09

[4] 87:01

[5] 3:169

[6] 66:11

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 106
  • Imechapishwa: 01/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy