al-Qummiy amesema wakati alipokuwa anafasiri Aayah:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يَشْتَرُونَ الضَّلَالَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّوا السَّبِيلَ

“Je, huoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu [hapo kabla] wanapendelea upotevu na wanataka mpotee njia… “[1]

 bi maana wale waliopotea kutokamana na kiongozi wa waumini:

وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّوا السَّبِيلَ

“… na wanataka mpotee njia.“

Bi maana kuwatoa watu kutoka katika uongozi wa kiongozi wa waumini ambayo ndio njia iliyonyooka.”[2]

Tazama namna ambavyo zindiki huyu anavyopotosha kwa uongozi huu uliyozuliwa na Ibn Sabaa´ na ambao unakataliwa na ´Aliy, familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waislamu wengine wote. ´Aliy alitaka kumuua myahudi huu kwa sababu ya uongo wake kukiwemo kwamba ´Aliy ndiye ambaye aliteuliwa baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini Raafidhwah hawawezi jengine isipokuwa kwenda kinyume na ´Aliy na waislamu wengine wote na kumfuata Ibn Sabaa´ na batili zake. Bali uhakika wa mambo ni kuwa Raafidhwah wamempiku kwa kiasi kikubwa na wamezikengeusha Aayah za Qur-aan kwa sababu ya uongo huu na kwa sababu ya kuwakufurisha Maswahabah na waumini wengine wote.

Enyi Raafidhwah! Allaah ameiteremsha Aayah hii kwa ajili ya kuwasema vibaya mayahudi, kuwaadhibu na kuwakafirisha. Kwa sababu wao wamemkufuru Allaah na Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa yale aliyokuja nayo. Wamekana ile bishara njema iliyokuja katika Tawraat kumuhusu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), sifa zake na sifa za Ummah wake. Nafsi zenu haziwezi kuipachika Aayah hii kwa mayahudi, hivyo badala yake mnaipachika kwa viumbe bora baada ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanawapenda sana watu hawa baada ya Mitume na shaytwaan na marafiki zake ndio wanaowachukia sana na kuwabughudhi.

Mayahudi, manaswara na Raafidhwah wanachotaka ni kuwapotosha Maswahabah na waumini wengine kutokamana na njia ya Allaah. Wakati huohuo Maswahabah walitaka kuwaongoza watu. Walipambana katika njia ya Allaah ili kuwaongoza watu katika njia ya Allaah iliyonyooka. Allaah aliwajaalia kufanya hivo hata kama Raafidhwah wanaona vibaya.

[1] 04:44

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/139).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 129
  • Imechapishwa: 07/11/2017