85. Wakati Muhammad ataposimama chini ya ´Arshi

83 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliletewa nyama sehemu ya mkono ikanyofolewa kwa ajili yake. Alikuwa anapenda kipande hicho. Akakata kipande hicho na kusema: ”Mimi ndiye bwana wa watu siku ya Qiyaamah… Kisha nitaondoka mpaka nifike chini ya ´Arshi, ambapo nianguke hali ya kumsujudia Mola wangu. Kisha kusemwe: ”Ee Muhammad, inua kichwa chako! Omba upewe, shufai usikizwe.” Niinue kichwa changu na kusema: ”Ummah wangu, ee Mola wangu.” Ndipo kusemwe: ”Ee Muhammad! Waingize ummah wako mlango wa kulia wa Peponi wale wasiokuwa na hesabu. Wanayo nafasi ya kutosha ya milango mingine yote ya Pepo kama walivyo wengine wote.”[1]

[1] Ahmad (02/435-436), al-Bukhaariy, Muslim na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 106
  • Imechapishwa: 01/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy