84. Wakati Muhammad alipoingia kwa Mola wake

82 – Anas ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Mimi ndiye mtu wa kwanza ambaye ardhi itamfufua siku ya Qiyaamah na si fakhari. Nitaenda kwenye mlango wa Pepo na kushika kengele yake, ambapo watasema: ”Ni nani?” Niseme: ”Ni Muhammad.” Nifunguliwe na kuingia ambapo nimkute al-Jabbaar mbele yangu, ambapo nimsujudie.”[1]

[1] Katika ile ya asili mtunzi ameipokea Hadiyth kupitia kwa al-Layth, kutoka kwa Ibn-ul-Haad, kutoka kwa ´Amr. Mpaka hapa wasimulizi ni wenye kuaminika na wenye kutambulika. Ikiwa wengine wote pia ni madhubuti na cheni ya wapokezi haina dosari, basi ni Swahiyh. Hadi hivi sasa sijapata cheni yake ya wapokezi katika zile tungo za asili za wanazuoni wa Hadiyth. Hata hivyo imebeba maana ya Hadiyth ya Thaabit iliyotangulia (12) kutoka kwa Anas, ambapo mtunzi amezingatia cheni yake ya wapokezi kuwa yenye nguvu. Ni ushahidi mzuri wa cheni hii. Aidha nimetaja nyingine yenye kuitia nguvu kutoka kwa Ibn ´Abbaas – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 105
  • Imechapishwa: 01/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy