81 – Amesema tena kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ
“Na kwa hakika amemuona katika uteremko mwingine.”[1]
”Mola Wake (´Azza wa Jall) alimkaribia.”
Cheni ya wapokezi ni nzuri[2].
[1] 53:13
[2] Ni kweli kwamba cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Ameipokea katika ile asili kupitia kwa Yahyaa bin Sa´iyd al-Umawiy: Muhammad bin ´Amr ametuhadithia, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas. Hivo ndivo imekuja katika chapa zote, kukiwemo muswada (2/19). Katika cheni ya wapokezi kunakosekana kiunganishi kati ya Yahyaa na Muhammad bin ´Amr. Kiunganishi hicho alikuwa ni baba yake na Yahyaa na alikuwa anaitwa Sa´iyd bin Abaan al-Umawiy. Ibn Jariyr katika tafsiri yake ya Qur-aan amepokea kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd al-Umawiy: Baba yangu ametuhadithia: Muhammad bin ´Amr ametuhadithia… Wapokezi wote walioko katika cheni ya wapokezi ni wenye kuaminika isipokuwa tu Muhammad bin ´Amr bin ´Alqamah bin Waqqaas al-Laythiy. Kuna maoni tofauti juu ya Muhammad bin ´Amr. Maoni ya mwisho ya wanazuoni ni kwamba masimulizi yake ni mazuri. Haafidhw Ibn Hajar ameashiria hilo pale aliposema:
”Mkweli mwenye kukosea.”
Hata hivyo masimulizi ya cheni yake ya wapokezi ni yenye kutofautiana. al-Umawiy ameyapokea namna hiyo kutoka kwa Ibn ´Abbaas. al-Fadhwl bin Muusa ameyapokea kutoka kwa Muhammad bin ´Amr: Kathiyr bin Hubaysh ametuhadithia, kutoka kwa Anas bin Maalik, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Wakati nilipokuwa nimelala msikitini… kisha akamsogelea mpaka akasimama.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”… kisha akamsogelea mpaka akasimama ambapo akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi.”
Ameipokea Ibn Khuzaymah katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd”, uk. 139-140, kwa tamko la kwanza. Ibn Jariyr ameipokea kupitia kwa an-Nadhwr bin Shumayl: Muhammad bin ´Amr bin´Alqamah bin Waqqaas al-Laythiy ametukhabarisha… (Jaamiy´-ul-Bayaan (27/27-28))
Kathiyr bin Hubaysh, ambaye pia akiitwa Kallad Khunays, ni mnyonge. Ikiwa Muhammad bin ´Amr ameihifadhi kutoka kwake, basi ni yenye kupingana na dhaifu kwa sababu itakuwa inaenda kinyume na yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwamba aliyesogea karibu alikuwa ni Jibriyl (´alayhis-Salaam). Kama alivopokea Ibn Jariyr kutoka kwa Masruuq, ambaye amesema:
”Nilimwambia ´Aaishah: ”Unasemaje juu ya:
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّى فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَى
“ … kisha akakurubia na akashuka; kisha akawa kiasi cha umbali wa ncha mbili au karibu zaidi.”?
´Aaishah akasema: ”Alikuwa ni Jibriyl. Alikuwa akimjilia kwa umbo la kiume. Mara hii alimjilia kwa umbo lake ambapo akafunika upeo wa mbingu.” (Jaamiy´-ul-Bayaan (27/28))
Muslim amepokea mfano wake. Inapingana na masimulizi ya Ibn ´Abbaas ya hivi upunde. Hapo ni pale ambapo yamethibiti kutoka kwake.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 104
- Imechapishwa: 01/07/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 104
Imechapishwa: 01/07/2024
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/83-mola-kumkaribia-muhammad/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)