84. Ni ipi hukumu ya kuweka changarawe juu ya kaburi na kunyunyizia maji?

Swali 84: Ni ipi hukumu ya kuweka changarawe juu ya kaburi na kunyunyizia maji?

Jibu: Imependekezwa ikiwa ni wepesi kufanya hivo. Ni mambo yanaufanya mchanga kuwa imara na kuulinda. Inasemekana kwamba imepokelewa kuwa kuliwekwa juu ya kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) changarawe. Imependekezwa kunyunyizia maji ili udongo uthibiti na kaburi libaki libaki wazi lisije kutwezwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 60
  • Imechapishwa: 01/01/2022