81 – Amesema tena kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ

“Na kwa hakika amemuona katika uteremko mwingine.”[1]

”Mola Wake (´Azza wa Jall) alimkaribia.”

Cheni ya wapokezi ni nzuri[2].

[1] 53:13

[2] Ni kweli kwamba cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Ameipokea katika ile asili kupitia kwa Yahyaa bin Sa´iyd al-Umawiy: Muhammad bin ´Amr ametuhadithia, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas. Hivo ndivo imekuja katika chapa zote, kukiwemo muswada (2/19). Katika cheni ya wapokezi kunakosekana kiunganishi kati ya Yahyaa na Muhammad bin ´Amr. Kiunganishi hicho alikuwa ni baba yake na Yahyaa na alikuwa anaitwa Sa´iyd bin Abaan al-Umawiy. Ibn Jariyr katika tafsiri yake ya Qur-aan amepokea kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd al-Umawiy: Baba yangu ametuhadithia: Muhammad bin ´Amr ametuhadithia… Wapokezi wote walioko katika cheni ya wapokezi ni wenye kuaminika isipokuwa tu Muhammad bin ´Amr bin ´Alqamah bin Waqqaas al-Laythiy. Kuna maoni tofauti juu ya Muhammad bin ´Amr. Maoni ya mwisho ya wanazuoni ni kwamba masimulizi yake ni mazuri. Haafidhw Ibn Hajar ameashiria hilo pale aliposema:

”Mkweli mwenye kukosea.”

Hata hivyo masimulizi ya cheni yake ya wapokezi ni yenye kutofautiana. al-Umawiy ameyapokea namna hiyo kutoka kwa Ibn ´Abbaas. al-Fadhwl bin Muusa ameyapokea kutoka kwa Muhammad bin ´Amr: Kathiyr bin Hubaysh ametuhadithia, kutoka kwa Anas bin Maalik, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Wakati nilipokuwa nimelala msikitini… kisha akamsogelea mpaka akasimama.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

”…  kisha akamsogelea mpaka akasimama ambapo akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi.”

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd”, uk. 139-140, kwa tamko la kwanza. Ibn Jariyr ameipokea kupitia kwa an-Nadhwr bin Shumayl: Muhammad bin ´Amr bin´Alqamah bin Waqqaas al-Laythiy  ametukhabarisha… (Jaamiy´-ul-Bayaan (27/27-28))

Kathiyr bin Hubaysh, ambaye pia akiitwa Kallad Khunays, ni mnyonge. Ikiwa Muhammad bin ´Amr ameihifadhi kutoka kwake, basi ni yenye kupingana na dhaifu kwa sababu itakuwa inaenda kinyume na yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwamba aliyesogea karibu alikuwa ni Jibriyl (´alayhis-Salaam). Kama alivopokea Ibn Jariyr kutoka kwa Masruuq, ambaye amesema:

”Nilimwambia ´Aaishah: ”Unasemaje juu ya:

ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّى فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَى

“ … kisha akakurubia na akashuka; kisha akawa kiasi cha umbali wa ncha mbili au karibu zaidi.”?

´Aaishah akasema: ”Alikuwa ni Jibriyl. Alikuwa akimjilia kwa umbo la kiume. Mara hii alimjilia kwa umbo lake ambapo akafunika upeo wa mbingu.” (Jaamiy´-ul-Bayaan (27/28))

Muslim amepokea mfano wake. Inapingana na masimulizi ya Ibn ´Abbaas ya hivi upunde. Hapo ni pale ambapo yamethibiti kutoka kwake.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 104
  • Imechapishwa: 01/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy