81. Malaika wanaoshuka kutoka kwa Allaah na kupanda Kwake

Dalili nyingine katika Sunnah zinazofahamisha ujuu wa Allaah, ni zile Hadiyth zinazotaja kuwa Malaika wanashuka kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kupanda Kwake. Mfano wa wale Malaika wanaohifadhi ambao wanashuka kila siku; wako ambao wanashuka alfajiri na kubaki pamoja nasi mpaka ´Aswr, wengine wakashuka ´Aswr na kubaki pamoja nasi mpaka alfajiri:

“Wanapishana kwenu Malaika wa usiku na Malaika wa mchana. Wanakusanyika katika swalah ya Fajr na swalah ya ´Aswr. Halafu hupanda wale waliolala kwenu ambapo Mola wenu Anawauliza – ilihali ni mjuzi zaidi kuliko wao: “Mmewaachaje waja Wangu?” Wanasema: “Tumewaacha na huku wanaswali na tumewaendea na huku wanaswali.”

Wanahesabu matendo ya wanadamu:

وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ كِرَامًا كَاتِبِينَ يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ

“Hakika juu yenu bila shaka kuna wenye kuhifadhi; watukufu wanaoandika. Wanajua yale myafanyayo.”[1]

[1] 82:10-12

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 118-119
  • Imechapishwa: 21/08/2024