Swali 112: Una nini cha kusema katika kuitukuza Sunnah na Ahl-us-Sunnah, kujifunza nayo na kuifanyia kazi pamoja na kuwachukia Bid´ah na watu wa Bid´ah?
Jibu: Kile ambacho ninajinasihi nafsi yangu na ndugu zangu ni kumcha Allaah (Ta´ala)[1], kushikamana barabara na mfumo wa Salaf na kujihadhari na Bid´ah na wazushi. Aidha watilia umuhimu kujifunza ´Aqiydah sahihi na yale yanayopingana nayo na kujifunza elimu kutoka kwa wanazuoni wanaoaminika katika elimu na ´Aqiydah yao.
Sambamba na hilo watahadhari kutokana na walinganizi waovu ambao wanaivisha haki batili na wanaificha haki ilihali wanaijua[2] au wajinga ambao wanajidai haki ilihali hawaijui[3], kwa sababu wanaharibu zaidi kuliko wanavotengeneza[4].
[1] Amesema (Ta´ala):
وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا اللَّـهَ
”Hakika Tumewausia wale waliopewa Kitabu kabla yenu na nanyi [pia tunakuusieni] kwamba: “Mcheni Allaah.” (04:131)
Amemwamrisha pia Mtume Wake na akasema:
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ اتَّقِ اللَّـهَ وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا
”Ee Nabii! Mche Allaah na wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa kila jambo, Mwenye hekima!” (33:1)
Amewaamrisha waumini na akasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ
“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na muaminini Mtume Wake… ” (57:28)
Amewaamrisha watu wote na akasema:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ
“Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni… ” (4:1)
[2] Hivo ndivo wanavofanya mayahudi. Wanaijua haki na wanajua kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume aliyetumilizwa na Allaah. Licha ya hivo wakamkadhibisha. Wao:
الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ
“… walioghadhibikiwa… .”
[3] Hivi ndivo walivo manaswara ambao wanamwabudu Allaah juu ya upotevu, pasi na elimu na umaizi. Wao ni:
الضَّالِّينَ
“… waliopotea!” (01:07)
´Abdullaah bin al-Mubaarak amesema:
”Waliopotea katika wanazuoni wetu wanafanana na mayahudi na waliopotea katika watu wetu wa kawaida wanafanana na manaswara.”
[4] ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) amesema:
”Yule mwenye kutenda pasi na elimu basi anaharibu zaidi kuliko anavotengeneza.” (Jaamiy´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih (54))
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 257-258
- Imechapishwa: 21/08/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
Swali 112: Una nini cha kusema katika kuitukuza Sunnah na Ahl-us-Sunnah, kujifunza nayo na kuifanyia kazi pamoja na kuwachukia Bid´ah na watu wa Bid´ah?
Jibu: Kile ambacho ninajinasihi nafsi yangu na ndugu zangu ni kumcha Allaah (Ta´ala)[1], kushikamana barabara na mfumo wa Salaf na kujihadhari na Bid´ah na wazushi. Aidha watilia umuhimu kujifunza ´Aqiydah sahihi na yale yanayopingana nayo na kujifunza elimu kutoka kwa wanazuoni wanaoaminika katika elimu na ´Aqiydah yao.
Sambamba na hilo watahadhari kutokana na walinganizi waovu ambao wanaivisha haki batili na wanaificha haki ilihali wanaijua[2] au wajinga ambao wanajidai haki ilihali hawaijui[3], kwa sababu wanaharibu zaidi kuliko wanavotengeneza[4].
[1] Amesema (Ta´ala):
وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا اللَّـهَ
”Hakika Tumewausia wale waliopewa Kitabu kabla yenu na nanyi [pia tunakuusieni] kwamba: “Mcheni Allaah.” (04:131)
Amemwamrisha pia Mtume Wake na akasema:
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ اتَّقِ اللَّـهَ وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا
”Ee Nabii! Mche Allaah na wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa kila jambo, Mwenye hekima!” (33:1)
Amewaamrisha waumini na akasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ
“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na muaminini Mtume Wake… ” (57:28)
Amewaamrisha watu wote na akasema:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ
“Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni… ” (4:1)
[2] Hivo ndivo wanavofanya mayahudi. Wanaijua haki na wanajua kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume aliyetumilizwa na Allaah. Licha ya hivo wakamkadhibisha. Wao:
الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ
“… walioghadhibikiwa… .”
[3] Hivi ndivo walivo manaswara ambao wanamwabudu Allaah juu ya upotevu, pasi na elimu na umaizi. Wao ni:
الضَّالِّينَ
“… waliopotea!” (01:07)
´Abdullaah bin al-Mubaarak amesema:
”Waliopotea katika wanazuoni wetu wanafanana na mayahudi na waliopotea katika watu wetu wa kawaida wanafanana na manaswara.”
[4] ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) amesema:
”Yule mwenye kutenda pasi na elimu basi anaharibu zaidi kuliko anavotengeneza.” (Jaamiy´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih (54))
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 257-258
Imechapishwa: 21/08/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/112-nasaha-kwa-ndugu-zetu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)