Swali 113: Ni vigezo vipi vilivyowekwa katika Shari´ah ambavyo vinatakiwa kuchukuliwa ili muislamu aweze kulazimiana navyo na kushikamana na mfumo wa Salaf na asipinde kutokana nayo na kuathirika na mifumo iliyopinda?
Jibu: Mosi mtu anatakiwa kuwarejea wanazuoni na watu wa utambuzi[1], ajiunze kutoka kwao na awatake ushauri yale anayoyafikiria ili aweze kutenda kwa mujibu wa maoni yao.
Pili ni kuwa mtu anatakiwa kuwa na utulivu na asiwe na asifanye haraka. Asiwe na papara ya kuwahukumu watu. Bali ni lazima kwake ahakikishe kwanza. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ
“Enyi walioamini! Anapokujieni fasiki kwa habari yoyote, basi pelelezeni msije mkawasibu watu kwa ujinga, mkawa kuwa wenye kujuta juu ya ambayo mmeyafanya.”[2]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا
”Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye jihaad, basi hakikini na wala msimwambie anayekuamkieni kwa salamu ´wewe sio muumini` kwa sababu ya kutamani mambo ya kidunia na ilihali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa hapo kabla na Allaah akakuneenemesheni, basi thibitisheni. Hakika Allaah kwa yale myatendayo ni Mjuzi daima wa Khabari za dhahiri na siri.”[3]
Bi maana thibitisheni juu ya yale yaliyokufikieni. Mkishahakikisha basi ni juu yenu kuyarekebisha kwa njia za kujenga na si kwa njia za jeuri au za usumbufu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Fanyeni wepesi na msifanye ugumu. Toeni bishara njema na wala msikimbize.”[4]
”Hapana vyenginevyo mmtumwa hali ya kuwa ni wenye kuwepesisha, na hamkutumwa hali ya kuwa ni wenye kutia ugumu.”[5]
”Hakika kuna katika nyinyi wenye kukimbiza. Yule anayewaongoza watu basi akhafifishe, kwani nyuma yake kuna wanyonge na watu wenye haja.”[6]
Mambo yanatakiwa kutengenezwa kwa hekima na utulivu. Haifai kwa kila mmoja kuingilia mambo ambayo hayawezi kuyashughulikia vilivyo.
Tatu mtu anatakiwa kujiongezea elimu yake kwa kuketi na wanazuoni, kuwasikiliza maoni yao na kusoma vitabu vya Salaf na historia za watengenezaji wa ummah huu na wanazuoni wake na ni namna gani walikuwa wakiyatengeneza mambo mbalimbali, wakiwawaidhi watu, wakiamrisha mema, wakikemea maovu na wakihukumu mambo mbalimbali. Yote haya yameandikwa katika wasifu na kumbukumbu zao:
لَقَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ
”Kwa hakika katika visa vyao kuna mazingatio kwa wenye akili.”[7]
Muislamu ni mmoja katika ummah huu. Ummah ni mkusanyiko wa waislamu kuanzia mwanzo wake mpaka kusimama kwa Qiyaamah. Muislamu anatakiwa kuwarejelea Salaf na maisha yao na ni namna gani walikuwa wakiyatatua mambo mbalimbali na afuate mwongozo wao. Asiwatazame watu wa papara na wajinga ambao wanawachochea watu pasi na elimu na utambuzi. Hii leo kuna vijitabu vingi, mihadhara na makala zinazotoka kwa watu ambao ni wajinga juu ya Shari´ah. Wanawachochea watu na kuwaamrisha watu kwa mambo ambayo hawakuamrishwa nayo na Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haijalishi kitu hata kama wamefanya hivo kwa malengo na nia njema. Kinachozingatiwa ni kule kupatia. Haki ni ile iliyoafikiana na Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Salaf. Kuhusiana na watu, mbali na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanapatia na kukosea. Kwa ajili hiyo usawa unatakiwa kufanyiwa kazi na kosa linatakiwa kuachwa.
[1] Wanazuoni na watu wa utambuzi ni wale waliochukua elimu yao kutoka kwa wanazuoni wakubwa wanaolingania katika Tawhiyd na mfumo wa Salaf. Elimu haichukuliwi kutoka kwa watu waliosoma kutoka kwa watu wenye mifumo ya kubomoa wanaopiga vita mfumo wa Salaf. Wala elimu haichukuliwi kutoka kwa waandishi na wafikiriaji. Wala elimi haichukuliwi kutoka kwa wadogo ambao hawajabobea ndani ya elimu na ufahamu wa Salaf.
[2] 49:6
[3] 4:94
[4] al-Bukhaariy (3274).
[5] al-Bukhaariy (217).
[6] al-Bukhaariy (672)
[7] 12:111
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 258-261
- Imechapishwa: 21/08/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 258-261
Imechapishwa: 21/08/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/113-ni-vipi-muislamu-atalazimiana-na-njia-ya-salaf/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)