Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
Pepo na Moto vimeumbwa. Vimeshaumbwa, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:
“Nimeingia Pepo na nimeona kasiri.”[1]
“Nimeona Kawthar.”[2]
“Nimetazama Pepo na kuona wakazi wake wengi ni… Nimetazama Moto na kuona wakazi wake wengi ni… “
Mwenye kudai kuwa havijaumbwa anaikadhibisha Qur-aan na Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Siamini kuwa mtu kama huyo anaamini Pepo na Moto.
MAELEZO
Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuamini kuwepo kwa Pepo na Moto na kwamba vimeshaumbwa hivi sasa. ´Aqiydah hiyo ni kutokana na dalili za wazi na zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa mfano Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nimeingia Pepo na nimeona kasiri.”[3]
Hii ni dalili ya kwamba ipo hivi sasa, na kwamba Allaah ameshaumba Pepo na Moto. Makazi yote mawili yapo sasa na yako wakazi wake. Pepo ni kwa ajili ya waumini. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ
”Itakurubishwa Jannah kwa wamchao Allaah… ”[4]
Moto ni makazi wa wapotofu:
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِلْغَاوِينَ
”…. utadhihirishwa moto uwakao vikali mno kwa wapotofu.”[5]
Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipopandishwa safari ya mbinguni aliona Pepo, starehe zilizomo ndani yake za milele na akaona makazi yake. Pia imethibiti kuwa aliona Moto sehemu yake inakula sehemu nyingine. Zote hizi ni dalili zilizothibiti zinazofahamisha kuwa Pepo na Moto vimeshaumbwa na vipo hivi sasa.
[1] al-Bukhaariy (3679).
[2] al-Bukhaariy (4964), Muslim (400) na Abu Ya´laa (3186).
[3] al-Bukhaariy (3679).
[4] 26:90
[5] 26:91
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 173-174
- Imechapishwa: 28/06/2026
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
Pepo na Moto vimeumbwa. Vimeshaumbwa, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:
“Nimeingia Pepo na nimeona kasiri.”[1]
“Nimeona Kawthar.”[2]
“Nimetazama Pepo na kuona wakazi wake wengi ni… Nimetazama Moto na kuona wakazi wake wengi ni… “
Mwenye kudai kuwa havijaumbwa anaikadhibisha Qur-aan na Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Siamini kuwa mtu kama huyo anaamini Pepo na Moto.
MAELEZO
Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuamini kuwepo kwa Pepo na Moto na kwamba vimeshaumbwa hivi sasa. ´Aqiydah hiyo ni kutokana na dalili za wazi na zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa mfano Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nimeingia Pepo na nimeona kasiri.”[3]
Hii ni dalili ya kwamba ipo hivi sasa, na kwamba Allaah ameshaumba Pepo na Moto. Makazi yote mawili yapo sasa na yako wakazi wake. Pepo ni kwa ajili ya waumini. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ
”Itakurubishwa Jannah kwa wamchao Allaah… ”[4]
Moto ni makazi wa wapotofu:
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِلْغَاوِينَ
”…. utadhihirishwa moto uwakao vikali mno kwa wapotofu.”[5]
Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipopandishwa safari ya mbinguni aliona Pepo, starehe zilizomo ndani yake za milele na akaona makazi yake. Pia imethibiti kuwa aliona Moto sehemu yake inakula sehemu nyingine. Zote hizi ni dalili zilizothibiti zinazofahamisha kuwa Pepo na Moto vimeshaumbwa na vipo hivi sasa.
[1] al-Bukhaariy (3679).
[2] al-Bukhaariy (4964), Muslim (400) na Abu Ya´laa (3186).
[3] al-Bukhaariy (3679).
[4] 26:90
[5] 26:91
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 173-174
Imechapishwa: 28/06/2026
https://firqatunnajia.com/80-pepo-na-moto-vipo-hivi-sasa/