80. Muislamu mjinga anayetumbukia katika shirki na halafu akatubia

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa kumi na tatu

Muislamu mjinga anayetumbukia katika shirki na halafu akatubia

Washirikina wana hoja tata nyingine ambayo wanajaribu kuijadili kwa kisa hiki. Wanasema: “Kwa hakika wana wa israaiyl hawakukufuru kwa hilo na hali hadhalika wale waliosema “Tufanyie Dhaat Anwaat!”, hawakukufuru. Tunawajibu kwa kusema: “Wana wa israaiyl hawakufanya hilo, na hali kadhalika waliomuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakufanya hilo. Na wala hakuna tofauti ya kwamba wana wa israaiyl hawakufanya hilo, na lau wangelifanya hilo wangelikufuru. Na wala hakuna tofauti ya kwamba wale aliowakataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lau wasingelimtii na wakachukua Dhaat Anwaatw baada ya makatazo, wangelikufuru. Na hili ndilo linalotakikana.

MAELEZO

Baadhi ya washirikina wamejengea hoja hii kuwa ni utata na wakasema kuwa si Maswahabah wala wana wa israaiyl hawakukufuru. Jibu ya hili ni kwamba si Maswahabah wala wana wa israaiyl hawakufanya kitu baada ya kukaripiwa na Mitume wawili watukufu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 90
  • Imechapishwa: 25/11/2023