al-Qa’nabi amesema:

“Niliwasikia wakisema kuwa Maalik aliishi miaka 89. Alikufa mnamo 179.

Ismaa´iyl bin Abi Uways amesema:

“Niliwauliza baadhi ya wanafamilia wa Maalik kuhusu kile alichokisema kabla ya kufa kwake. Wakasema kwamba alitamka shahaadah na akasoma:

لِلَّـهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ

”Amri ni ya Allaah pekee kabla na baada.”[1]

Alikufa asubuhi ya tarehe 14 Rabiy´ al-Awwal 179. Mwanamfalme ´Abdullaah bin Muhammad bin Ibraahiym bin Muhammad bin ´Aliy bin ´Abdillaah bin ´Abbaas al-Hashimiy akamswalia swalah ya jeneza. Alikuwa mtoto wa Zaynab bint Sulayman al-Abbaasiyyah na anayejulikana kwa mama yake.”

Ameipokea Muhammad bin Sa’d, ambaye amesema:

”Nilimuuliza Musw’ab, ambaye alisema kwamba alikufa katika Safar. Ma´n bin ´Asaa alinifahamisha hayohayo.”

Abu Musw’ab az-Zuhriy amesema:

“Alifariki baada ya siku ya kumi ya Rabiy’ al-Awwal 179.”

Muhammad bin Suhnuun amesema:

“Alifariki tarehe 11 Rabiy’ al-Awwal.”

Ibn Wahb amesema:

“Alifariki ziliposalia siku kumi na tatu za Rabi’ al-Awwal.”

al-Qaadhwiy ´Iyaadhw amesema:

“Maoni sahihi ni kwamba alifariki baada ya ugonjwa wake siku ya Jumapili, tarehe 22 Rabiy’ al-Awwal.”

adh-Dhahabiy amesema:

“Kumepokelewa mapokezi mengi mno kwamba alikufa mnamo 179, yasizingatiwe maoni ya waliokosea kwamba alikufa mnamo 178. Vivyohivyo inaweza kusemwa juu ya maoni ya mwandishi wake Habiyb na Mutwarrif kwamba alikufa mnamo 180.”

al-Qaadhwiy ´Iyaadhw amemnukuu Asad bin al-Furaat:

“Nilimuota Maalik baada ya kufa kwake. Alikuwa amevaa nguo ndefu, za kijani. Alikuwa ameketi juu ya ngamia-jike na akaruka kati ya mbingu na nchi. Nikamwambia: “Ee Abu ´Abdillaah! Je,   hujafa?” Akasema: “Ndiyo.” Nikasema: “Ni nini kimetokea?” Akasema: “Nilifika kwa Mola wangu na Akanisemeza moja kwa moja. Akaniambia: “Niombe, Nitakupa. Tamani, Nitakuridhia.”

Allaah amrehemu, amsamehe na amkaze Pepo ya daraja la juu kabisa.

[1] 30:4

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 27/11/2025