8. Bid´ah ni mbaya zaidi kuliko madhambi makubwa

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚوَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae; na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa hakika amepotoka upotofu wa mbali kabisa.” (04:116)

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“Ni nani dhalimu zaidi kuliko yute anayemtungia Allaah uongo ili apoteze watu pasi na elimu? Hakika Allaah hawaongozi watu madhalimu.” (06:144)

لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ

“Ili wabebe mizigo [ya madhambi] yao kamili Siku ya Qiyaamah na mizigo ya wale waliowapoteza bila ya elimu – Zindukeni! Uovu ulioje wanayoyabeba.” (16:25)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu Khawaarij:

“Popote mnapokutana nao basi waueni. Ikiwa nitakutana nao basi nitawaua kama walivyouawa kina ´Aad.”[1]

Kumepokelewa [Hadiyth] Swahiyh ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kupambana na viongozi madhalimu muda wa kuwa wanaswali[2].

Jariyr bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa kuna mtu aliyetoa swadaqah na watu wakawa wamemuigiliza. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Yule mwenye kuhuisha katika Uislamu msingi mzuri basi ana ujira wake na ujira wa yule atakayeifanya baada yake pasi na kupungua chochote katika ujira wao. Na yule mwenye kuhuisha katika Uislamu msingi mbaya basi ana madhambi yake na madhambi ya yule atakayeifanya pasi na kupungua chochote katika madhambi yao.”[3]

Ameipokea Muslim ambaye amepokea tena mfano wa Hadiyth kama hiyo kupitia kwa Abu Hurayrah:

“Yule mwenye kuita katika uongofu…” na “Yule mwenye kuita katika upotevu…”[4]

[1] al-Bukhaariy (3611) na Muslim (1066).

[2] Muslim (1854).

[3] Muslim (1017).

[4] Muslim (2674).

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-ul-Islaam, uk. 25-27
  • Imechapishwa: 23/10/2016