Swali 79: Je, ni katika kuleta mkusanyiko kati ya waislamu kudharau baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa na kuwatuhumu kujikombakomba na kuwa ni vibaraka?

Jibu: Ni lazima kuwashimu wanazuoni wa Kiislamu kwa sababu wao ndio warithi wa Mitume. Kuwadharau kunahesabika ni kuzidharau nafasi zao, urithi wao wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ile elimu waliyoibeba. Ambaye anawadharau wanazuoni basi kwa wepesi kabisa atawadharau waislamu wengine. Kwa hivyo ni lazima kuwaheshimu wanazuoni kutokana na elimu yao, nafasi zao katika ummah na yale majukumu waliyoyabeba kwa ajili ya manufaa ya Uislamu na waislamu. Ikiwa hawaaminiwi wanazuoni ni nani ambaye ataaminiwa? Ukiondoka uaminifu juu ya wanazuoni waislamu watarejea kwa nani katika kuyamaliza matatizo yao na kuzibainisha hukumu za Shari´ah? Hakimu anapojitahidi na akapatia, basi anapata ujira mara mbili. Na anapojitahidi na akakosea, basi anapata ujira mara moja na lile kosa linasamehewa. Hakuna yeyote aliyewadharau wanazuoni isipokuwa ameiweka nafsi yake katika khatari ya kuadhibiwa. Historia ni ushahidi bora juu ya hilo, khaswa ikiwa wanazuoni hawa wamepewa jukumu ya kuyaangalia mambo yanayowahusu waislamu, kama vile mahakimu na kamati ya Kibaar-ul-´Ulamaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 200-202
  • Imechapishwa: 21/07/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy