Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيد

”Ni Uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, Mwenye kuhimidiwa.”[1]

وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ

“Na wale Tuliowapa Kitabu wanajua kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako kwa haki.”[2]

Zipo Aayah zingine nyingi mfano wa hizo ambazo kuhesabika kwake ni kwa tabu.

MAELEZO

Kushuka inakuwa kutokea kwa juu. Kwa hivyo ikafahamisha kuwa Allaah yuko juu, kwa sababu Qur-aan imeteremshwa kutoka Kwake. Sentesi kama:

تَنزِيلٌ

”Ni Uteremsho… “

مُنَزَّلٌ

”… kimeteremshwa… “

na:

أَنزَلَ إِلَيْكَ

“… Alichokuteremshia… “[3]

zinazojulisha ujuu wa Allaah. Kuna Aayah nyingi mfano wake zinazofahamisha kuwa Allaah (´Azza wa Jall) yuko juu ya viumbe na kwamba amelingana juu ya ´Arshi Yake. Ni Aayah nyingi mno, ambazo kujumlishwa kwake ni kwa tabu. Ndio maana wanasema kuwa kuna takriban dalili elfu zinazofahamisha Allaah kuwa juu.

[1] 41:42

[2] 6:114

[3] 04:166

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 115-116
  • Imechapishwa: 21/08/2024