Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atakuwa na Hodhi siku ya Qiyaamah, maji yake ni meupe zaidi kuliko maziwa, matamu zaidi kuliko asali na vikombe idadi yake ni sawa na nyote za mbinguni. Mwenye kunywa humo mara moja, basi hatohisi kiu baada yake kamwe.

MAELEZO

Hodhi maana yake kilugha ni kukusanya. Mtu husema hivo kwa kuachia na akakusudia maji yaliyokusanyika sehemu moja. Hodhi maana yake katika Shari´ah ni hodhi ya maji yanayoteremka ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka katika mto wa al-Kawthar katika uwanja wa siku ya Qiyaamah. Imefahamisha juu yake Sunnah iliyopokelewa kwa mapokezi mengi na Ahl-us-Sunnah wakaafikiana nayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika mimi nitakutangulieni katika hodhi.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

Salaf ambao ni Ahl-us-Sunnah wameafikiana juu ya kuthibiti kwake.

[1] al-Bukhaariy (6583, 6584) na Muslim (2290, 26, 2291, 26).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 123-124
  • Imechapishwa: 30/11/2022