77. Fir´awn anataka kupanda juu kumtafuta Mungu wa Muusa

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَ أَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا

“Ee Haamaan nijengee mnara ili nifikie njia; njia za mbinguni ili nimchungulie Mungu wa Muusa, kwani hakika mimi namdhania ni mwongo.”[1]

MAELEZO

Kisa cha Fir´awn na kiburi chake na kwamba alimwambia Haamaan:

ابْنِ لِي صَرْحًا

“Nijengee mnara… “

Anataka mnara mrefu ili apande juu yake na amtafute Allaah. Hii inajulisha kuwa Muusa (´alayhis-Salaam) alimweleza Fir´awn kuwa Allaah yuko juu ya mbingu. Fir´awn akataka kumkadhibisha na kujionyesha mbele za watu katika kumkadhibisha Muusa kwa njia ya kwamba atapanda juu ya mnara, amtafute Allaah na hivyo awadanganye watu na kuwaonyesha watu uwongo wa Muusa (´alayhis-Salaam).

[1] 40:36-37

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 115
  • Imechapishwa: 20/08/2024