Swali 110: Wanadai baadhi ya watu kuwa Salafiyyah ni kama makundi mengine yote yalioko leo na hukumu yake ni kama hukumu ya makundi mengine yote. Wasemaje kuhusiana na madai haya?
Jibu: Hili ni kama tulivyosema kwamba Salafiyyah ndio kundi lililo katika haki. Nalo ndio ambalo ni wajibu kujinasibisha nalo na kufanya nalo kazi. Makundi mengine yote hayazingatiwe kuwa ni makundi ya ulinganizi, kwa sababu yanakwenda kinyume. Vipi tutafuata kundi liendalo kinyume na Ahl-us-Sunnah na uongofu wa Salaf? Kundi liendalo kinyume na Salafiyyah ni kundi linaenda kinyume na mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake.
Kusema kuwa Salafiyyah ni kama makundi mengine yote ya Kiislamu ni kosa[1]. Salafiyyah ndio kundi pekee ambalo ni wajibu kulifuata, kupita katika mfumo wake, kujiunga nalo na kupigana Jihaad bega kwa bega nalo. Haijuzu kwa muislamu kujiunga na kundi lingine kwa sababu linaenda kinyume. Kuna mtu anaridhia kujiunga na wanaoenda kinyume? Muislamu haridhii hili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Lazimianeni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza. Ziumeni kwa magego yenu. Na nakutahadharisheni na mambo yaliyozuliwa, kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu kundi lililookoka:
”Mayahudi wamegawanyika makundi sabini na moja. Manaswara wamegawanyika makundi sabini na mbili. Na Ummah wangu utagawanyika katika mapote sabini na mbili. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: ”Ni lipi hilo, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: ”Ni lile linalofuata yale ninayofuata mii hii leo na Maswahabah zangu.”[3]
Je, hivi kweli mtu atataka kuokoka kisha ashike njia isiyokuwa yake?
Unataraji kuokoka na umeshika njia isiyo?
Hakika safina haipiti nchi kavu
[1] Shaykh Bakr Abu Zayd amesema:
”Baadhi ya wale ambao wameandika kuhusu makundi ya Kiislamu ya leo wamewataja Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kati wao. Hili ni kosa kubwa katika ufahamu na kufikiria kwao na kuwa mbali kutokana na uhakika wa mambo. Kwani Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni Ahl-ul-Hadiyth na wao ndio mkusanyiko wa waislamu. Wanasimamia Uislamu kikamilifu, tofauti na makudi mengine ambayo ni mapote.” (Hukm-ul-Intimaa’, uk. 115)
[2] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (34). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2455).
[3] Ibn Maajah (3992), at-Tirmidhiy (2641) na Abu Daawuud (4596). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Mishkaat-ul-Maswaabiyh” (171).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 254-256
- Imechapishwa: 20/08/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 254-256
Imechapishwa: 20/08/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/110-si-kama-makundi-mengine/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)