Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

64 – Atakuwa mwenye wasiwasi, mwenye kupotea na mwenye mashaka. Si muumini mwenye kusadikisha wala mwenye kukanusha na kukadhibisha.

MAELEZO

Hii ndio hali ya wenye mashaka na wanafiki. Daima wanakuwa wenye mashaka. Daima wanakuwa wenye kusita, daima wanakuwa wenye kuyumbayumba. Kwa sababu hawako imara katika Uislamu, hawakujisalimisha kwa Allaah wala kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema kuhusu wanafiki:

مُّذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَٰلِكَ لَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ وَلَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا

”Wenye kuyumbayumba kati ya hayo, huku hawako wala huko hawako. Na ambaye Allaah amempotoa huwezi kumpatia njia [ya yeye kuongoka].”[1]

وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ

“Wanapokutana na wale walioamini wanasema: “Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao pamoja na mashaytwaan wao wanasema: “Hakika sisi tupamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwachezea shere tu. Allaah anawachezea shere wao na atawaendeleza katika hali yao ya upindukiaji mipaka wa kuasi, wakitangatanga kwa upofu.”[2]

[1] 4:143

[2] 2:14-15

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 84
  • Imechapishwa: 23/01/2023