76. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kumi na nne wa Aal ´Imraan

al-´Ayyaashiy amesema:

“Muhammad bin Yuunus ameeleza kutoka kwa baadhi ya wenzetu waliosema: “Abu Ja´far amenieleza:

كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ او منشورة

“Kila nafsi itaonja mauti au itafufuliwa.”[1]

hivi ndivyo ilivyoteremka kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna yeyote katika Ummah huu isipokuwa atafufuliwa. Kuhusu waumini watafufuliwa wakiwa na furaha na waovu watafufuliwa hali ya kuwa Allaah amewatweza.”[2]

Mwongo huu anamaanisha kuwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio ambao wameondosha “au itafufuliwa” kutoka kwenye Aayah. Raafidhwah wanamaanisha kuwa wao ni waovu wataofufuliwa katika hali ya Allaah kuwatweza ilihali Raafidhwah wao ndio waumini ambao watafufuliwa hali ya kuwa na furaha. Hivi ndivyo wanavyofanya wapotevu na watu wenye vifundo.

[1] 03:185

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/210).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 115
  • Imechapishwa: 13/04/2017