75. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kumi na tatu wa Aal ´Imraan

al-´Ayyaashiy amesema:

“´Abdus-Swamad bin Bashiyr ameeleza kutoka kwa Abu ´Abdillaah aliyesema: “Hivi mnajua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikufa au aliuawa? Allaah amesema:

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِن مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ

“Muhammad si chochote isipokuwa ni Mtume tu [na] wamekwishapita kabla yake Mitume [wengine]. Je, akifa au akiuawa mtageuka nyuma ya visigino vyenu?”[1]

Alipewa sumu kabla ya kufa. Wale wawili ndio walimpa sumu kabla ya kufa.” Ndipo tukasema: “Wale wawili na baba zao ndio viumbe wawili waovu kabisa aliowaumba Allaah.”[2]

Mtenda dhambi huyu anawalenga wakeze Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye ni ´Aaishah na Hafswah (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Wachafu hawa wanasema kuwa Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ndio viumbe wawili waovu kabisa alioumba Allaah. Hivi kweli mayahudi na manaswara wamefikia katika aina ya uchafu kama huu na chuki dhidi ya Maswahabah wa Mitume wao na khaswa wale vigogo wao kama Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhum)?

Mabwana wenu wa kiyahudi ndio ambao walimpa sumu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakusema uongo na wala hakuzua juu ya wenzake. Sidhani kuwa yeye na mayahudi wamefikia moja ya kumi ya chuki mlionayo dhidi ya Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao ndio viumbe bora kabisa baada ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam).

[1] 03:144

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/200).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 114-115
  • Imechapishwa: 13/04/2017