75. Matamshi ya Tashahhud – Tamko la Abu Muusa al-Ash´ariy

4- Tashahhud ya Abu Muusa al-Ash´ariy. Abu Muusa ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mnapokaa chini basi kitu cha kwanza kusema kiwe:

التحيات الطيبات الصلوات لله ،[وحده لا شريك له]السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته، السلام علينا و على عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله و أشهد أن محمداً عبده و رسوله

“Maadhimisho, mazuri na swalah zote zinamstahikia Allaah [hali ya kuwa yupekee, hana mshirika]. Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume! Amani ishuke juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”

[Maadhimisho katika swalah yana maneno nane.”][1]

[1] Muslim, Abu ´Awaanah, Abu Daawuud na Ibn Maajah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 142
  • Imechapishwa: 01/01/2019