285 – Yuusuf bin Muusa ametukhabarisha: Jariyr ametukhabarisha, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye nadhani kuwa amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Watu wawili wenye tamaa hawatosheki: Mtu mwenye tamaa ya kutafuta elimu ambaye kamwe tamaa yake haikomi, na mtu mwenye tamaa ya kutafuta mali za dunia ambaye kamwe tamaa yake haikomi.”[1]

286 – al-Hasan bin ´Aliy al-Hulwaaniy na Muhammad bin Yahyaa wametukhabarisha: ´Abdus-Swamad bin ´Abdil-Waarith ametuhadithia: Haashim al-Kuufiy ametukhabarisha, kutoka kwa Zayd al-Khath´amiy amekhabarisha, kutoka kwa Asmaa’ bint ´Umays, ambaye amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Ni ubaya uliyoje wa mja ambaye anaidhuru dini kwa dunia yake.”[2]

287 – Wahb bin Baqiyyah ametukhabarisha, Khaalid ametukhabarisha, kutoka kwa  ´Abdur-Rahmaan, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Msishindane.”

288 – Husayn bin al-Aswad ametuhadithia: Abu Usaamah ametukhabarisha: ´Umar bin Hamzah ametukhabarisha, kutoka kwa Naafiy´, kutoka kwa Maalik bin Sahl, kutoka kwa Anas, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“´Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah’ huwakinga waja dhidi ya ghadhabu za Allaah maadamu hawapendelei maisha yao ya kidunia mbele ya dini yao. Wanapopendelea maisha yao ya kidunia mbele ya dini yao na wakasema `Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`, hurudiwa na Allaah (‘Azza wa Jall) akasema: “Mnasema uwongo.”[3]

Mpaka hapa ndipo mwisho wa kitabu. Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, Mola wa walimwengu wote. Ee Allaah! Msifu na umsalimu Muhammad na jamaa zake. Namuomba Allaah atujaalie tukisoma na kukifanyia kazi na asikifanye kiwe dhidi yetu. Aamiyn, ee Mola wa walimwengu wote! Allaah amrehemu mtunzi wake na mwandishi wake, mwenye kukisoma na mwenye kukifanyia kazi. Aamiyn, ee Mola wa walimwengu wote!

[1] Abu Khaythamah katika “Kitaab-ul-´Ilm” (141). al-Albaaniy amesema:

“Inatiwa nguvu kupitia njia nyingi ambazo baadhi yake zimesahihishwa na al-Haakim na adh-Dhahabiy.” (Kitaab-ul-´Ilm, uk. 56)

[2] at-Tirmidhiy (2448), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni ngeni na cheni yake ya wapokezi si yenye nguvu. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2448).

[3] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “adh-Dhwa´iyfah” (6301).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 75-76
  • Imechapishwa: 27/07/2025