72. Uislamu uleule, waislamu ndio wameharibika

278 – Fadhwl bin Sahl bin al-A´raj ametukhabarisha: Abu Ahmad az-Zubayriy ametukhabarisha: ´Abdul-Jabbaar bin al-´Abbaas ametukhabarisha, kutoka kwa ´Awn bin Abiy Juhayfah: Simjui mtu mwingine yeyote zaidi ya baba yangu aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtafunguliwa dunia, mpate mzipambe nyumba zenu kama inavyopambwa Ka’bah.” Tukasema: ”Je, tutakuwa na dini yetu kipindi hicho?” Akasema: ”Mtakuwa na dini yenu kipindi hicho.” Tukasema: ”Je, sisi kipindi hicho tutakuwa bora kuliko tulivyo leo?” Akasema: “Bali nyinyi hii leo ni bora.”[1]

279 – Muhammad bin ´Aliy bin Maymuun ametukhabarisha: Muusa bin Ayyuub ametukhabarisha: Makhlad bin Yaziyd ametukhabarisha, kutoka kwa Bashiyr, kutoka kwa Sayyaar, kutoka kwa Twaariq bin Shihaab, kutoka kwa Ibn Mas´uud, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Qiyaamah kinakaribia. Watu hawazidishi chochote kwa dunia isipokuwa tamaa na dunia haiwazidishii chochote isipokuwa kuwafanya wawe mbali zaidi.”

280 – Ibn Kaasib ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Muusa ametukhabarisha, kutoka kwa Usaamah bin Zayd, kutoka kwa ´Abdullaah bin Diynaar, kutoka kwa bwana mmoja katika Answaar, kutoka kwa Sa´d, ambaye ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Mwisho wa zama watakuwepo watu ambao wanakula dunia kwa ndimi zao vile ng’ombe anavyoramba kwa ulimi wake.”

281 – Abu Muusa ametukhabarisha: Wahb bin Jariyr ametukhabarisha: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia Yahyaa bin Ayyuub akisimulia kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Marthad, kutoka kwa ´Uqbah bin ´Aamir, ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi sichelei kwamba  mtashirikisha baada yangu – lakini nachelea kwamba mtashindana, kupigana vita na muangamie.”[2]

282 – al-Maqdamiy ametukhabarisha: Bishr bin al-Mufadhdhwal ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Ishaaq, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Anas, ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Msishindane.”

283 – Ibn ´Awf ametukhabarisha: Abu Ghassaan ametukhabarisha, kutoka kwa Qays, kutoka kwa Shamr bin ´Atwiyyah, kutoka kwa Shihr bin Hawshab, kutoka kwa ´Amr bin ´Absah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Itapofika siku ya Qiyaamah, dunia itasogezwa mbele. Kitenganishwe kutokana nayo kile ambacho kilifanywa kwa ajili ya Allaah, na kile ambacho kilifanywa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah kitatupwa ndani ya Moto wa Jahannam.”[3]

284 – Ibn Swadraan ametukhabarisha: Buzaygh Abul-Khayl al-Khasswaaf ametukhabarisha: al-A´mash ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Waa-il, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Itafika kwa watu wakati wanakaa kwenye msikiti duara kwa duara na wanaongozwa na dunia. Msiketi nao, kwa sababu Allaah hana haja nao.”[4]

Ibn Swadran amesema:

“Nilimuuliza Abu Hafsw as-Swayrafiy: “Je, ulileta chochote kutoka Buzaygh?” Akasema: “Alikuwa akisema kwamba alizungumza sokoni … niliyaandika kutoka kwake.” Nikamwambia Sulaymaan (yaani ash-Shaadhukaaniy), ambaye akasmea: “Ameandika nini kutoka kwenye Hadiyth hii?”

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3614).

[2] al-Bukhaariy (1344) na Muslim (2296).

[3] Dhaifu yakiwa ni maneno ya ´Amr bin ´Absah kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (5).

[4] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (1163).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 73-75
  • Imechapishwa: 27/07/2025