Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

125 – Hatumsadikishi kuhani, mpiga ramli wala yeyote anayedai kitu kinachoenda kinyume na Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Ummah.

126 – Tunaona mkusanyiko ndio haki na usawa, na mgawanyiko ni upindaji na adhabu.

MAELEZO

Nayo ni yale aliyokuwemo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Nao ni Kundi lililookoka, Ahl-ul-Hadiyth na wale wengine wote watakaofuata njia yao katika wafuasi wa madhehebu na wenigeneo.

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 108
  • Imechapishwa: 27/10/2024