Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

”Bali Allaah alimnyanyua Kwake. Allaah ni Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye hekima.”[1]

مِّنَ اللَّـهِ ذِي الْمَعَارِجِ تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ

“… kutoka kwa Allaah Mwenye njia za kupandia. Malaika na Roho wanapanda Kwake katika siku kadiri yake ni miaka khamsini elfu.”[2]

MAELEZO

Malaika hushuka ardhi kisha wakapanda juu kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa maamrisho ya Allaah. Wanashuka ardhini kwa amri ya Allaah:

وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ

”Na hatuteremki ila kwa amri ya Mola wako.”[3]

Kinacholengwa katika Aayah ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko juu, kwa sababu Malaika wanapanda Kwake.

[1] 4:158

[2] 70:3-4

[3] 19:64

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 111
  • Imechapishwa: 19/08/2024