Swali 108: Unawanasihi nini vijana ambao wamedanganyika na makundi haya, wakajiunga nao na wakalingania kwao?
Jibu: Tunawahimiza vijana wote na khaswa vijana wa nchi hii wajiunge na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na Kundi lililookoka linalowakilishwa na wanazuoni wa nchi hii, viongozi na watu wa kawaida. Wote wameleleka juu ya Tawhiyd na wakapita juu ya njia sahihi. Sisi hali yetu iko wazi[1].
Tunawahimiza vijana wafuate kundi hili ambalo linapita juu ya mfumo sahihi na wasiangalie mapote, makundi, vyama na wahalifu wengine. Mambo hayo yatafanya kuondoshwa neema katika nchi yetu na kutenganisha umoja wetu na mioyo yetu, kama mambo yalivyo hii leo kwa masikitiko.
Uhasama huu uliopo kati ya vijana wa leo na wengi ambao wanajinasibisha na ulinganizi katika nchi hii unatokana na kuyaangalia makundi haya, kudanganyika nayo na kueneza fikiria zake. Hii ndio sababu ya uhasama uliopo kati ya vijana na baadhi ya wanafunzi. Endapo wangelishukuru neema ya Allaah iliopo juu yao na wakashikamana na ule utambuzi na ulinganizi uliofanyiwa kazi na kusimamishwa na muhuishaji Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah), basi wasingeangalia mapote haya yanayoenda kinyume kutokana na yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah wake na wale waliowafata kwa wema. Ulinganizi wa Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) una zaidi ya miaka 200 na bado umefaulu. Hakuna yeyote aliyepingana nao na unapita juu ya njia sahihi.
Hapana shaka kuwa nchi imesimama juu ya Qur-aan na Sunnah na ulinganizi ni wenye kufaulu. Mpaka maadui wamelikubali hilo. Maadui wamekubali kuwa nchi hii ndio nchi bora zaidi ulimwenguni inayoishi katika utulivu, amani na usalama. Kila mmoja analikiri hili. Ni kwa nini tunataka kubadilisha neema hii na tukatazamia fikira za wengine ambazo hazikufaulu katika nchi zao? Fikira, ulinganizi na makundi haya hayakufaulu katika nchi zao wala kulea kundi lililote linalotengeneza. Nchi zao hazikubalikika kutoka kuwa nchi za kisekula, za kishirikina, kuyaabudia makaburi na kwenda katika nchi za Kiislamu sahihi. Kwa sababu makundi haya hayaipatilizi ´Aqiydah na ndio maana hayakufaulu. Ni kwa nini basi tunastaajabishwa nayo, tunayaeneza na kulingania kwayo?
[1] Baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa liliandika:
”Tunatahadharisha aina zote za kujiunga katika fikira zilizopinda na kulazimiana na makundi na mapote ya kigeni. Watu wote wa nchi hii wanapaswa kuwa wamoja wenye kushikamana na Salaf, wale waliowafuatia na yale waliyokuwemo wakati wote maimamu wa Uislamu katika kulazimiana na Mkusanyiko, nasaha za kweli na kuacha kutengeneza kasoro au kuzieneza.” (at-Twaa’if, kongamano 39, 1413)
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 252-254
- Imechapishwa: 19/08/2024
- taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 252-254
Imechapishwa: 19/08/2024
taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
https://firqatunnajia.com/108-hapa-ndipo-kulizuka-uhasama-kati-ya-vijana-na-wanafunzi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)