Swali 109: Ni kwa nini Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wameitwa hivo?

Jibu: Ahl-us-Sunnah wameitwa hivo kwa sababu wanazitendea kazi na kulazimiana na Sunnah. Wameitwa al-Jamaa´ah, Mkusanyiko, kwa sababu wamekusanyika na hawatengani. Kwa sababu mfumo wao ni mmoja; Qur-aan na Sunnah. Aidha wamekusanyika juu ya haki na kwa mtawala mmoja. Ni wamoja, wenye kusaidiana na wenye kupendana katika mambo yao yote ya kijumla.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 254
  • Imechapishwa: 19/08/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy