271 – Abu Swaalih Hadiyyah bin ´Abdil-Wahhaab al-Marwaziy ametuhadithia: an-Nadhwr bin Shumayl ametukhabarisha: Abu Nu´aamah al-´Adawiy ametukhabarisha: Abu Hunaydah al-Baraa’ bin Nawfal ametukhabarisha, kutoka kwa Waalaan, kutoka kwa Hudhayfah, kutoka kwa Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mambo yote ya kidunia na Aakhirah, yatayokuwepo mpaka siku ya Qiyaamah, yalionyeshwa kwangu.”[1]
272 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ishaaq bin Sulaymaan ar-Raaziy ametukhabarisha: Mughiyrah bin Muslim ametukhabarisha, kutoka kwa Farqad as-Sabkhiy, kutoka kwa Murrah at-Twayyib, kutoka kwa Abu Bakr as-Swiddiyq, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hatoingia Peponi mtu mwenye tabia mbaya kwa wale anaowamiliki.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Si ulituambia kuwa ummah huu ndio wenye watumwa na wajane wengi kuliko mataifa mengine?” Akasema: “Ndiyo, basi wakirimuni kama mnavyowakirimu watoto wenu na walisheni katika vile mnavyokula ninyi wenyewe.” Wakasema: “Ni kitu gani kinachotufaa kutoka duniani?” Akasema: “Farasi unayemfunga kwa ajili ya kupigana katika njia ya Allah na mtumwa anayeshughulikia haja zako. Ikiwa anaswali, basi huyo ni ndugu yako mara mbili.”[2]
273 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ibn Numayr ametukhabarisha, kutoka kwa as-Swabbaah bin Muhammad al-Ahmasiy, kutoka kwa Murrah al-Hamadaaniy, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule anayetaka Aakhirah basi huacha mapambo ya dunia.”[3]
274 – Abu Bakr ametuhadithia: Ibn Numayr ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Mu´aawiyah an-Naswriy (ambaye alikuwa madhubuti) ametuhadithia, kutoka kwa Nahshal, kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin Muzaahim, kutoka kwa al-Aswad, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesema:
“Mwenye kufanya hamu yake yote ni jambo moja, basi Allaah atamtosheleza kutokana na jambo la Aakhirah yake. Na yule ambaye hamu yake imeparanganyika juu ya dunia, basi Allaah hajali ni kwenye bonde gani la ardhi ataangukia.”[4]
275 – Abu Bakr ametukhabarisha: Mu´aawiyah bin Hishaam ametukhabarisha, kutoka kwa ´Aliy bin Swaalih, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Sisi watu wa Nyumba Allaah ametuchagulia Aakhirah mbele ya dunia.”[5]
276 – Abu Bakr ametukhabarisha: al-Hasan bin Muusa ametukhabarisha: Ibn Lahiy´ah ametukhabarisha: Abul-Aswad ametukhabarisha kwamba amemsikia Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan bin Labiybah akihadithia kutoka kwa Abu Sinaan, kutoka kwa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Allaah hamfungulii yeyote maisha ya dunia isipokuwa Allaah ataweka uadui na chuki baina yao mpaka siku ya Qiyaamah.”[6]
277 – Muhammad bin Ismaa´iyl ametukhabarisha: ´Iysaa bin Ibraahiym al-Baswriy ametukhabarisha: ´Abdul-´Aziyz bin Muslim ametukhabarisha: Matwar al-Warraaq ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Nadhwrah, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy, ambaye amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alitutolea Khutbah baada ya ‘Aswr na akasema: “Jihadharini na dunia na jihadharini na wanawake.”[7]
[1] Ahmad (16). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (3641).
[2] Ibn Maajah (3691). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (6340).
[3] at-Tirmidhiy (2458). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2458).
[4] Ibn Maajah (257). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (6189).
[5] Ibn Maajah (4082). Dhaifu na inayopingana kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “adh-Dhwa´iyfah” (5205).
[6] Ahmad (93). Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa Ahmad Shaakir na dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy “adh-Dhwa´iyfah” (4871).
[7] al-Bukhaariy (5096) na Muslim (2741).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 72-73
- Imechapishwa: 27/07/2025

Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 72-73
Imechapishwa: 27/07/2025
https://firqatunnajia.com/71-yule-anayetamani-aakhirah-huiacha-dunia/