Yakishabainika hayo basi utaona namna ilivyo khatari kwa yale waliyotahiniwa nayo wengi katika wale matajiri wa Kiislamu hii leo ambapo wanawaajiri wanawake wa kikafiri katika majumba yao, kwa sababu kuna uwezekano kwa mume na mke, au mmoja wao, kuingia ndani ya mtihani na kwenda kinyume na Shari´ah. Mtihani wa mume ni jambo liko wazi kwa sababu anaweza kutumbukia ndani ya uzinzi, khaswa kwa kuzingatia kwamba wanawake wa kikafiri hawajichungi na machafu na yaliyo halali na yaliyo haramu katika maisha yao. Hayo yametamkwa wazi na Qur-aan kuhusu wanawake wa watu wa Kitabu – kusemwe nini kuhusu hali ya waabudia masanamu ambao hawana Kitabu? Vilevile ni vigumu mno wale wake wa hii leo na wasichana waliobaleghe kujisitiri mbele ya wale wafanyakazi wao majumbani kama wanavyojisitiri mbele ya wanamme wa kando nao. Waliosalimika ni wachache miongoni mwa wale waliokingwa na Allaah. Na endapo tutakadiria kuwa mume na mke watasalimika kutokana na mtihani, basi hawatosalimika watoto wao kuathirika na maadili na desturi zao zinazopingana na dini yetu. Hapa ni pale ambapo hawatokuwa na makusudio ya kuharibu malezi ya watoto na kuwatia mashaka juu ya dini yao, kama tulivyosikia yanafanywa na baadhi yao.

Aidha nimesikia kutoka kwa mmoja katika wale wanaotoa fatwa – ikiwa ni kweli ni jukumu linarudi kwa yule msimulizi – ambaye amejuzisha kuwatumia wafanyakazi hawa majumbani na akawafananisha na wale wajakazi wanaofaa kutumiwa. Nakhofia mtu kama huyu kidogo kidogo atahalalisha kufanya nao jimaa kwa kutumia mantiki hiyohiyo, khaswa kwa kuzingatia kwamba wako ambao wameondosha adhabu ya Kishari´ah kwa kufanya uzinzi na wale wafanyakazi wa nyumbani – hata kama wanawake hao watakuwa waislamu – kwa kujengea hoja kuwa wamewaajiri!?!?

Haya ndio niliyopenda kuwabainishia watu juu ya suala hili. Huenda Allaah akamnufaisha kwayo ambaye pengine ameghafilika nayo na ambaye amepuuza kuyatendea kazi. Naye (Subhaanah) ndiye Mwenye kuongoza katika njia ilionyooka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 116-117
  • Imechapishwa: 10/10/2023