70. Sura ya tisa: Mtazamo wa kilimwengu na uharibifu unaopatikana ndani yake II

Miongoni mwa mitazamo ya kidunia ya maisha haya ni yale Allaah aliyotaja katika kisa cha Qaaruun na zile hazina alizompa Allaah:

فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ

“Akajitokeza kwa watu wake katika pambo lake. Wale wanaotaka uhai wa dunia wakasema: “Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruun, hakika yeye ana fungu kuu.”[1]

Wakatamani mfano wake na wakamfanya ni mwenye bahati na tena wakamsifu kuwa na sehemu kubwa kutokana na mtazamo wao wa kidunia. Hali ni kama hivi katika nchi za kikafiri na maendeleo walionayo ya viwanda na uchumi. Wale waislamu wenye imani dhaifu wanalitazama jambo hilo kwa mtazamo wa kushangazwa pasi na kuzingatia ule ukafiri waliyomo na yale mafikio mabaya yanayowasubiri. Mtazamo huu wa kimakosa ukafuatiwa na kuwatukuza makafiri, kuwaheshimu ndani ya nafsi zao, kujifananisha nao katika tabia na desturi zao mbaya na hawakuwaigiliza katika kuzifanya nguvu zikawa mpya, kuwaandalia nguvu hizo na  baadhi ya manufaa katika kuvumbua na kuunda. Amesema (Ta´ala):

وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ

“Waandalieni nguvu zozote mziwezazo.”[2]

[1] 28:79

[2] 08:60

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 135-136
  • Imechapishwa: 06/04/2020