Aidha mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema kuwa inatakiwa kuamini Kuonekana pasi na kuifanyia namna. Usiulize ni vipi Allaah ataonekana. Kama zilivyo sifa nyingine zote za Allaah (´Azza wa Jall) hatujui namna ya Kuonekana. Tunaamini Kuonekana, tunajua maana yake na tunaithibitisha, lakini pamoja na hivyo hatujui namna ilivyo. Allaah (Subhaanah) ndiye anajua zaidi namna itakavyokuwa.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 79
- Imechapishwa: 17/01/2023