Watu haohao wanajengea hoja pia kwa Aayah isemayo:

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي

“Alipokuja Muusa katika miadi Yetu na Mola wake akamsemesha, [Muusa] alisema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” Akasema: “Hutoniona, lakini tazama mlima ukitulia mahali pake basi utaniona.”[1]

Kwa mujibu wao wanasema ni dalili inayopinga Kuonekana. Hata hivyo Aayah inahusu duniani. Muusa aliomba kumuona duniani. Hakuna yeyote amuonae Allaah duniani, si Mitume wala wengine. Kuhusu Aakhirah waumini watamuona Mola wao. Hali ya ulimwenguni sio kama hali ya Aakhirah. Ulimwenguni watu ni wanyonge katika miili na fahamu zao. Hawawezi kumuona Allaah (´Azza wa Jall) duniani. Ama Aakhirah Allaah atawapa nguvu na hivyo wataweza kumuona Mola wao – huko ni kuwakirimu. Kwa ajili hiyo pindi Muusa (´alayhis-Salaam) alipomuomba Allaah kumuona alimwambia:

لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا

“Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” Akasema: “Hutoniona! Lakini tazama jabali, likitulia mahali pake, basi utaniona.” Basi Mola wako alipojidhihirisha katika jabali, alilijaalia kuwa lenye kupasukapasuka.”[2]

Mlima ulisambukasambuka na ukageuka vumbi. Vipi kuhusu mtu ambaye ameumbwa kwa nyama, damu na mifupa ataweza kumuona Allaah duniani? Hapana shaka kwamba hawezi kumuona duniani. Isitoshe maombi ya Muusa (´alayhis-Salaam) ni dalili ya uwezekano wa kuonekana kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa sababu Muusa hawezi kumuomba Mola wake kitu kisichojuzu. Alimuomba kitu kinachojuzu lakini hata hivyo hilo halitokuwa duniani. Kwa ajili hiyo ndio maana akasema:

لَن تَرَانِي

“Hutoniona!”

Hakusema kuwa Yeye haonekani. Allaah ataonekana Aakhirah na watu wenye haki zaidi ya uonekanaji huu ni Mitume.

[1] 7:143

[2] 7:143

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 78-79
  • Imechapishwa: 17/01/2023