Kujiunga na makundi ya kipindi cha kikafiri na ubaguzi wa kitaifa ndio ukafiri mwingine na kuritadi kutoka nje ya Uislamu. Kwani Uislamu umeutupilia mbali ubaguzi wa kitaifa na wa kipindi cha kikafiri. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana namwanamme na mwanamke na tukakujaalieni  mataifa na makabila mbalimbali ili mtambuane. Hakika mbora zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni yule mwenye kumcha Allaah zaidi kati yenu.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si katika sisi yule anayeita katika ubaguzi, si katika sisi anayepigana kutokana na ubaguzi na si katika sisi yule anayeghadhibika kwa ajili ya ubaguzi.”[2]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika Allaah amewaondosheeni kiburi cha kipindi cha kikafiri na kujifakhirisha kwa kina baba. Si vyeninevyo ima [mtu akawa] ni muumini mchaji au muovu aliyekula maangamivu. Watu ni wana wa Aadam na Aadam ameumbwa kutokana na udongo. Hakuna ubora kwa mwarabu juu ya asiyekuwa mwarabu isipokuwa kwa uchaji.”[3]

Isitoshe ukundikundi huu unawafarikisha waislamu. Allaah ameamrisha umoja na kukusanyika juu ya wema na kumcha Allaah na akakaripia kutengana na kufarikiana. Amesema (Ta´ala):

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا

“Shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane. Ikumbukeni neema ya Allaah juu yenu pindi mlipokuwa maadui kisha akaunganisha nyoyo zenu mkawa kwa neema Yake ndugu.”[4]

Hakika Allaah anatutaka tuwe pamoja na kundi moja ambalo ni kundi la Allaah waliofaulu. Lakini ulimwengu wa Kiislamu, baada ya Ulaya kuwapiga vita kisiasa, kiutamaduni, kitaifa na kinchi, wamekuwa ni wenye kunyenyekea ubaguzi huu wa kidamu na wakiuamini kama utasema ni qadhiya ya kisomi na yenye uhakika iliyothibitishwa. Matokeo yake raia wake [nchi hizo] wakawa na msukumo wa juu kabisa wa kuhuisha ubaguzi huu uliofishwa na Uislamu, kuimba kwao, kuhuisha nembo zake na kujigamba kwa wakati wake uliotangulia kabla ya Uislamu, jambo ambalo Uislamu uliliondoa na kuliita “Jaahiliyyah” na Allaah amewatunuku waislamu kutoka katika jambo hilo na akawasisitiza kuishukuru neema hii.

Kimaumbile muumini hataji kipindi cha kikafiri kilichotangulia au kilichokaribu isipokuwa kwa kukichukia na mwili wake husisimka. Hivi mtu aliyetoka jela baada ya kuadhibiwa, kudhulumiwa na kunyanyaswa akikumbuka zile siku ngozi yake si husisimka? Hivi mtu aliyepona kutoka katika magonjwa yaliyomchukua muda mrefu akakaribia kupatwa na mauti akikumbuka zile siku za maradhi si akili yake hufunikwa na rangi yake hubadilika? Lililo la wajibu ni kutambua kuwa makundimakundi haya ni adhabu. Allaah ameyaagiza kwenda kwa yule mwenye kuipa mgongo Shari´ah Yake na akaiacha dini Yake.  Amesema (Ta´ala):

قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ

“Sema: “Yeye ni muweza wa kukutumieni adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu au akutatanisheni mfarikiane kuwa makundimakundi na akuonjesheni baadhi yenu nguvu za wengineo.”[5]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muda wa kuwa viongozi wao hawatohukumu kwa Kitabu cha Allaah isipokuwa Allaah atafanya ni wenye kugombana kati yao.”[6]

Kuwa na ushabiki kwa vikundivikundi inapelekea kuikataa haki ilioko kwa wengine kama ilivyo hali ya mayahudi ambao Allaah amesema kuwahusu:

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا نُؤْمِنُ بِمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ وَهُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَهُمْ

“Pindi wanapoambiwa: “Aminini yale aliyoyateremsha Allaa wanasema: “Tunaamini yale yaliyoteremshwa kwetu na wanayakanusha yale yaliyokuja baada yake na hali ya kuwa hayo ni haki yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao.”[7]

Vilevile kama ilivyo hali ya watu wa kipindi cha kikafiri ambao waliikataa haki aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ajili ya kushabikia yale waliyokuwemo baba zao:

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا

“Wanapoambiwa: “Fuateni aliyoyateremsha Allaah husema: “Bali tunafuata tuliyowakuta nayo baba zetu.”[8]

Watu wa vikundivikundi hivi malengo yao wanachotaka ni kuyafanya badala ya Uislamu ambao Allaah amemtunuku nao mwanadamu.

[1] 49:13

[2] Abu Daawuud (5121).

[3] Ahmad (8721), Abu Daawuud (5116) na at-Tirmidhiy (3964).

[4] 03:103

[5] 06:65

[6] Ibn Maajah (4019).

[7] 02:91

[8] 02:170

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 130-132
  • Imechapishwa: 31/03/2020