68. Adhabu au neema na starehe ni kwa roho na kiwiliwili vyote viwili

Je, adhabu au neema za kaburi ni juu ya roho au ni juu ya mwili? Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Madhehebu ya Salaf wa Ummah na maimamu wake ni kwamba adhabu inaipata ile roho ya maiti na kiwiliwili chake na kwamba roho baada ya kutengana na kiwiliwili inabaki hali ya kuwa ni yenye kustareheshwa au kuadhibiwa na kwamba wakati fulani inawasiliana na kiwiliwili na hivyo inafikiwa na neema na starehe au adhabu.”[1]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (04/282).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 114
  • Imechapishwa: 28/11/2022